Feb 18, 2026

Tanzania Reports Tripling of Clean Cooking Access at IEA High-Level Ministerial Dialogue

 

Tanzania has more than tripled access to clean cooking energy within four years, Energy Minister Hon. Deogratius Ndejembi announced at a High-Level Ministerial Dialogue convened by the International Energy Agency (IEA).

National access increased from 6.9% in 2021 to 23.2% in 2025, reflecting accelerated policy action aimed at expanding clean, safe and affordable cooking solutions. The transition supports improvements in public health, environmental sustainability and economic productivity.

Jan 27, 2026

MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO YAPANDA MITI AINA YA OLORIEN, MITI MAARUFU WAKATI WA TOHARA KWA VIJANA WA KIMASAI.


Na Mwandishi Wetu, Ngorongoro.

Tofauti na vijana wa mjini hasa wa Dar es Salaam ambao wengi wao hutahiriwa wakiwa wadogo hospitalini  tena kwa ganzi, tohara kwa vijana wa kimasai hufanyika wakiwa mabarobaro na mashabaro na tena bila ganzi na hivyo kusikia maumivu makali ya kitendo hicho.

Katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeungana naye kwa kupanda miti aina ya Olorien katika kijiji cha Oloirobi Wilayani Ngorongoro.

Miti hiyo hukatwa na hutumika mara baada ya vijana wa kimasai kufanyiwa Jando/kutahiriwa, kijana akishatahiriwa miti huo huwekwa mlangoni wa nyumba yenye kijana aliyetahiriwa kisha akina mama huzunguka ulipowekwa mti husika huku wakiimba kwa furaha na vigelegele kuashiria kwamba zoezi la tohara limefanyika na kukamilika.

Jan 15, 2026

NGORONGORO SHOWCASES TANZANIA’S PREMIER SAFARI EXPERIENCE AT MAGISTRATES’ AND JUDGES’ CONFERENCE IN DODOMA

 

The Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA) has joined the Annual General Meeting of the Tanzania Magistrates and Judges Association in Dodoma, leveraging the high-level national platform to amplify destination marketing, spotlight world-class tourism offerings, and strengthen strategic collaboration between Ngorongoro and the Judiciary.

Officially opened on 13 January 2026 by the President of the United Republic of Tanzania, H.E. Dr. Samia Suluhu Hassan, the conference runs through 16 January 2026, convening legal sector stakeholders from across the country to deliberate on matters of justice, the rule of law, and the continued strengthening of Tanzania’s justice delivery system.

Jan 7, 2026

BODI YA ZABUNI NGORONGORO YAONGEZEWA UJUZI WA UTENDAJI KAZI.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) imeendelea kuwajengea uwezo watumishi wake katika maeneo mbalimbali ambapo kwa sasa inaendesha  mafunzo maalum ya siku 5 kuanzia tarehe 5-9 Januari 2026 kwa wajumbe wa bodi ya zabuni (Tender Board) ili kuwaongezea ujuzi zaidi katika utekelezaji wa  majukumu yao.

Dec 4, 2025

VIKUNDI VYA KINAMAMA VYAWEZESHWA NA NGORONGORO KUFANYA ZIARA YA MAFUNZO NDANI YA HIFADHI.

Na Mwandishi wetu, Ngorongoro.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kupitia Idara ya Maendeleo ya Jamii imewawezesha  wakinamama 84 kutoka Kata ya Ganako, wilayani Karatu, kufanya ziara ya mafunzo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro baada ya kupewa mafunzo ya kutengeneza majiko banifu ili kulinda mazingira 

Ziara hiyo ni sehemu ya programu ya elimu kwa vitendo inayolenga kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na matumizi ya teknolojia rafiki na kuepuka kukata miti na matumizi ya mkaa kwa jamii inayozunguka hifadhi ya Ngorongoro.

Akizungumza katika ziara hiyo, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Bi. Lightness Kyambile, amesema hatua hiyo inalenga kuwawezesha wanawake kuwa mabalozi wa uhifadhi katika jamii zao ili kuepuka kukata miti, kuchoma mkaa na kuharibu mazingira.

Dec 1, 2025

WANANCHI WA ORMEKEKE NGORONGORO WAANZA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI


Wananchi wa Kitongoji ya Ormekeke Kijiji cha Nasipaoriong tarafa ya Ngorongoro wameanza kunufaika na mradi wa maji baada ya Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuchimba kisima chenye uwezo wa kuzalisha lita 13,00 kwa saa na kujenga tanki  lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita 135,000 kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo.

Akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa kukamilika kwa mradi huo kümeleta  manufaa makubwa  kwa wananchi wa maeneo ya Ormekeke, Nasipaoriong na Olduvai yaliyopo hifadhi ya Ngorongoro ambao kipindi cha kiangazi walilazimika kuhamishia mifugo maeneo ya mengine kufuata maji

Nov 26, 2025

TANZANIA, KOREA KUONGEZA KASI YA UCHUMI

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Korea zimefungua ukurasa mpya wa ushirikiano wa kiuchumi kupitia Jukwaa la Biashara la Tanzania–Korea (Tanzania–Korea Business Forum) lililowakutanisha wadau wa uwekezaji na biashara wa serikali na sekta binafsi kutoka mataifa yote mawili.

Akifungua jukwaa hilo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), amesema Tanzania na Korea zinaunganishwa na dira ya pamoja ya ustawi, ubunifu na maendeleo ambayo ndio msingi wa kukuza ushirikiano wa kiuchumi baina ya mataifa hayo. 

 

Mhe. Kombo ameongeza kuwa licha ya kukua kwa biashara kati ya Tanzania na Korea, bado upo uwanda mkubwa wa kuongeza ushirikiano huo haswa katika eneo la bidhaa za chakula, viwanda vya vifungashio na usindikaji wa bidhaa. 

Nov 20, 2025

ELIMU YA UHIFADHI SHIRIKISHI NA KUHAMASISHA UTALII MASHULENI YAENDELEA KUTOKA MAMLAKA YA HIFADHI NGORONGORO

Na Mwandishi Wetu, Karatu

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imeendelea na programu ya kutoa elimu ya uhifadhi shirikishi na kuhamasiha utalii wa ndani kwenye shule mbalimbali ambapo leo tarehe 20 Novemba, 2025  watumishi wa Mamlaka hiyo wametembelea Shule ya Sekondari Banjika iliyopo Karatu  Mkoani Arusha.

Katika ziara hiyo, wataalam wa uhifadhi na utalii walitoa elimu kuhusu umuhimu wa uhifadhi, vivutio vya utalii vilivyopo Ngorongoro, pamoja na nafasi ya wanafunzi  kuwa mabalozi wa utalii na uhifadhi ikiwemo kuanzisha klabu za uhifadhi wa mazingira. 

Nov 12, 2025

UJUMBE KUTOKA CHUO CHA TAIFA CHA ULINZI (NDC -TANZANIA) WAFANYA ZIARA YA MAFUNZO MAMLAKA YA HIFADHI YA ENEO LA NGORONGORO.

Na Mwandishi Wetu, Karatu

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi ( NDC) Balozi Meja Jenerali W.A. Ibuge ameongoza wakufunzi na Wanafunzi kutoka mataifa 17, kutembelea eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kwa kuanzia jengo la makumbusho ya Jiopaki ( Urithi Geo- Museum) kwa ziara ya utalii na kimafunzo.

Ujumbe huo umejifunza mambo mbalimbali kuhusu vivutio vya utalii, shughuli za uhifadhi,  kijiolojia na urithi wa utamaduni yanayopatikana katika eneo la Ngorongoro na maeneo yanayozunguka hifadhi hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Balozi Meja Jenerali Ibuge alisema:

“Tumefurahi kutembelea makumbusho haya ya kipekee na kisasa ambayo yanaonesha utofauti na upekee wa Ngorongoro ukilinganisha na maeneo mengine.

Nov 7, 2025

KAMISHNA BADRU UHIFADHI NDIO NGUZO PEKEE KATIKA SEKTA YA UTALII;

 

Na Mwandishi wa NCAA, Karatu.

Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) Bw. Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa kusimamia na kuendeleza uhifadhi ni jukumu la msingi kwa mamlaka hiyo  kwani uhifadhi  ndiyo moyo katika ustawi wa utalii na maendeleo ya jamii.

Akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro katika ofisi za makao makuu Karatu Arusha tarehe 7 Novermba, 2025 Kamishna Badru amesisitiza kuwa, usimamizi madhubuti wa rasilimali za wanyamapori, Misitu na Malikale zilizopo hifadhi ya Ngorongoro ni jambo la kufa na kupona na kueleza watumishi hao kuwahudumia wageni wanaotembelea hifadhi kwa wakati, ukarimu, uadilifu na nidhamu ili kuendelea kulinda chapa ya Ngorongoro (Brand) kama eneo bora la utalii wa kifahari (Premium  Safari Destination)

Nov 4, 2025

Fake News Alert: President Ibrahim Traoré Did Not Turn Down Invitation from President Samia Suluhu


A viral post circulating on social media claiming that Burkina Faso President Ibrahim Traoré turned down an invitation from Tanzania’s President Samia Suluhu Hassan to attend her “military inauguration” in Dodoma has been confirmed to be false.

Reliable sources from Tanzania’s Ministry of Foreign Affairs, who requested anonymity due to the sensitivity of diplomatic matters, have clarified that no such invitation was ever extended to President Traoré or any official delegation from Burkina Faso.

Furthermore, the official stated clearly that the inauguration took place at the statehouse in a civil televised official ceremony in accordance to Tanzania laws and constitution.  

The official further explained that Tanzania continues to uphold strong diplomatic relations with other African nations, including Burkina Faso, but any insinuation of strained ties between the two countries is completely fabricated.

The post, which appears to originate from a page labeled #KenyaDailyReport and dated 03/11/2025, has spread widely on social media. However, no credible media outlet in either Tanzania or Burkina Faso has reported on such an incident.

Oct 24, 2025

JENERALI MABEYO (MST) ATETA NA MAKAMISHNA WASAIDIZI WAANDAMIZI WA UHIFADHI NGORONGORO AKAZIA UADILIFU NA KUCHAPA KAZI

Kassim Nyaki, NCAA.

Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Jenerali Venance Mabeyo (Mst) amewavisha cheo makamishna wasaidizi waandamizi wa uhifadhi wawili na kuwahimiza Kuchapa kazi, uadilifu, kutimiza wajibu, kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza utendaji kazi katika utumishi wa Umma.


Waliovishwa Cheo  baada ya kuhitimu mafunzo ya Jeshi la Uhifadhi ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Brown O.  Shimwela anayesimamia Idara ya fedha pamoja na Kamishna msaidizi Mwandamizi Dkt. Amani Makota anayesimamia Idara ya TEHAMA na Takwimu.

Oct 17, 2025

ALUMNI WA SHULE YA SEKONDARI KIBAHA WAZINDUA KAMPUNI

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Mh. Abdul Mombokaleo, Oktoba 16, 2025 amezindua rasmi KISSAN COMPANY LIMITED, katika mahafali ya 57 ya kidato cha nne katika shule ya Sekondari Kibaha.

Kuzinduliwa kwa kampuni hiyo inayoundwa na baadhi ya wahitimu wa zamani wa shule ya Sekondari Kibaha (Kibaha Alumni), kunalenga kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuchangia maendeleo ya nchi, hasa eneo la kuboresha elimu na mazingira ya kusomea nchini.

Awali kabla ya kuanzishwa kwa KISSAN, Alumni hao, tarehe 24/04/2025, wakiambatana na aliyekuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita ambaye pia ni Alumni wa Kibaha Sekondari, Mh. Mombokaleo, waliipatia shule hiyo Kompyuta 20 na vifaa vyake  na kuwezesha upatikanaji wa mtandao (internet) kwa mwaka mzima.  

Oct 16, 2025

MAKUMBUSHO YA KISASA YA URITHI WA JIOLOJIA YAZINDULIWA NGORONGORO NA MAKAMU WA RAIS DKT. MPANGO

Na Mwandishi wetu, Karatu Arusha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip  Isdor Mpango, leo tarehe 16, 2025, amezindua Makumbusho ya kisasa ya Jiolojia ya Ngorongoro-Lengai (Urithi Geo Museum) baada ya mradi huo kukabidhwa na Serikali ya China kwa Serikali ya Tanzania katika eneo la  Karatu mkoani Arusha. 

Mradi huo  uliogharimu shilingi Bilioni 32 ni msaada kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ambao ulilenga kuboresha miundombinu ya utalii, ujenzi wa makumbusho ya kisasa ya jiolojia na kuendeleza shughuli za uhifadhi katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na maeneo mengine ya hifadhi ya jiolojia ya Ngorongoro-Lengai (Ngorongoro-Lengai Geopark Development Project)

Oct 15, 2025

DKT NATU AKUTANA NA WAKURUGENZI WA IMF JIJINI WASHINGTON

 


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, DKT. Natu El-maamry Mwamba (kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa( IMF) , Bw. Adran Ubisse, baada ya kikao chao kilichofanyika Makao Makuu ya Taasisi hiyo, Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambapo katika mazungumzo yao Bw. Ubisse aliipongeza Tanzania kwa kuwa na rekodi nzuri ya utekelezaji wa miradi kwa kutumia vizuri fedha inazokopa.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, DKT. Natu El-maamry Mwamba (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa( IMF) , Bw. Adran Ubisse ( wa pili kulia), Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil (wa pili kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Kanza (wa kwanza kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao kilichofanyika makao makuu ya IMF, jijini Washington D.C, nchini Marekani.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, DKT. Natu El-maamry Mwamba (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anayesimamia Idara ya Afrika, Bw. Abebe Selassie (wa pili kulia), Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil (wa pili kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Kanza (wa kwanza kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao kilichofanyika makao makuu ya IMF, jijini Washington D.C, nchini Marekani.




Oct 9, 2025

NI FURAHA ZAIDI MRADI WA MAJI KUNUFAISHA WANANCHI WA HIFADHI YA NGORONGORO

Na Mwandishi wetu, Ndutu Ngorongoro

Tarehe 9 Oktoba, 2025.

Wananchi wa kata za Endulen, Alaetoli na Kakesio zilizopo eneo la Hifadhi ya Ngorongoro wanatarajiwa kunufaika na mradi wa maji unaotekelezwa na Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi  ya Ngorongoro ambapo kwa kata ya Endulen kisima chenye urefu wa mita 250  chenye uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita za maji 80,000 kwa siku kimechimbwa katika eneo la Mlima Matiti kata ya Endulen. 

Akiwa katika ziara ya kukagua ujenzi wa mradi huo ambao utekelezaji wake upo zaidi ya 50%, Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka  ya Hifadhi ya Ngorongoro Bw. Abdul-Razaq Badru ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo utasaidia wananchi wa kata za Endulen, Alaetoli, Kakesio na baadae Olbalbal ili kukabiliana na changamoto ya upungufu wa maji kwa mifugo hasa msimu wa kiangazi.

“Hapa kata ya Endulen baada utafiti tumepata maji ya kutosha, kisima kilichochimbwa katika eneo hili kitazalisha lita 8,000 kwa saa na lita laki moja (100,000) kwa siku, tunaamini ndani ya wiki moja majaribio ya mwisho ya kujaza maji yatakuwa yamekamilika, mabwawa ya kukusanya maji yatachimbwa na mifugo zaidi ya 2000 itakuwa inapata maji hapa kila siku,” alifafanua Badru

Sep 22, 2025

NCAA NA POLISI WAADHIMISHA SIKU YA FARU DUNIANI


Maadhimisho ya siku Faru Duniani ambapo leo tarehe 22 Septemba 2025 Maafisa na Askari wa Hifadhi ya Ngorongoro kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Karatu, wadau wa Uhifadhi na Utalii na Wananchi wameungana katika Mbio za kilomita 5 katika mji wa Karatu zenye lengo la kuhamasisha shughuli za uhifadhi wa Mnyama Faru.

Kauli Mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Faru ni "Tuhakikishe aina tano za Faru waliopo duniani wanaishi"

Sep 19, 2025

DKT. ABBASI AFUNGUA MAFUNZO KUHUSU ELIMU YA UTALII WA ANGA KWA WADAU WA UTALII.

Kassim Nyaki, Karatu.

19 Septemba, 2025.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi amefungua mafunzo ya siku tatu kuhusu elimu ya utalii wa anga (astrotourism) yaliyoanza leo tarehe 19 Septemba, 2025 Karatu Mkoani Arusha.

Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) yanatolewa na wataalamu wabobezi kutoka taasisi za Astrotourism Aotearoa (AAA) kutoka nchini New Zealand, Smithsonian Astrophysical Observatory (SAO) ya Chuo Kikuu cha Harvard  pamoja na taasisi ya kimataifa ya Dark Sky International yenye Makao Makuu Jijini Arizona, Marekani.

Akifungua mafunzo hayo Dkt. Abbas amesema utoaji wa mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Wizara ya Maliasili na utalii kufungua mazao mapya utalii ikiwepo utalii wa Anga ambapo hatua ya sasa ni kutoa mafunzo, maarifa na ujuzi kwa watanzania kuhusu utalii wa anga, vifaa vinavyotumika na fursa zilizopo katika aina hiyo ya utalii. 

Sep 18, 2025

DKT. ABBASI AKAGUA UJENZI WA MAKUMBUSHO YA JIOLOJIA (GEOPARK) KARATU


Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi leo Septemba 18, 2025 ametembelea na kukagua ujenzi wa Makumbusho ya Jiolojia (Geopark) mjini Karatu.

Akizungumza baada ya ukaguzi wa jengo hilo Dkt. Abbasi ameiagiza Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kuboresha baadhi ya historia zilizohifadhiwa katika jengo hilo ili zisomeke kwa usahihi zaidi.

Sep 17, 2025

Exploring the Depths of History: A Journey into Amboni Caves


By Our Correspondent, Tanga

The air is thick with excitement as students from Alharamain High School in Dar es Salaam and Alfagems Secondary, joined by visitors from different corners of Tanzania and even beyond the country, step into the cool darkness of the Amboni Caves in Tanga.


What begins as a school trip quickly turns into something bigger, a shared adventure. Inside the caves, voices echo off ancient limestone walls, laughter blends with curiosity, and flashlights light up formations that seem sculpted by time itself. Some marvel at the silence, others whisper about the stories and legends tied to the caves, and many simply stand in awe at the thought of walking where generations before them once stood.

Sep 10, 2025

TANZANIA YAORODHESHWA KATIKA NCHI ZINAZOTAZAMIWA KUFUZU KUTOKA NCHI MASIKINI

Na. Peter Haule na Joseph Mahumi, WF, Dodoma

Tanzania imeorodheshwa na Kamati ya Sera za Maendeleo ya Umoja wa Mataifa, kuwa miongoni mwa nchi zinazotazamiwa kufuzu kutoka katika kundi la nchi masikini (Least Developed Countries) kwenda nchi inayoendelea.

 

Hayo yamebainishwa jijini Dodoma na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, wakati wa Mkutano wa Awali wa tathmini ya nchi kutoka nchi maskini kwenda nchi inayoendelea inayofanywa na Umoja wa Mataifa (UN) kupitia Shirika lake la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD).

 


Dkt. Mwamba alisema hatua hiyo imetokana na Tanzania kupiga hatua kubwa katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika kipindi cha miongo miwili iliyopita kupitia uthabiti wa Sera za uchumi zilizosababisha kukua kwa uchumi kwa wastani wa asilimia 6.2 kati ya mwaka 2000 na 2024.

WAZIRI KOMBO AKUTANA NA KATIBU MKUU WA IMO KUIMARISHA USHIRIKIANO WA MASUALA YA BAHARI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo amekutana kwa mazungumzo na Katibu Mkuu wa Shirika la Bahari Duniani (IMO), Bw. Arsenio Domínguez, jijini London.

Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na IMO hususan katika nyanja za usalama wa baharini, ulinzi, utunzaji wa mazingira ya bahari na kujengeana uwezo.

Mhe. Waziri Kombo alieleza jinsi Serikali ya Tanzania inavyothamini ushirikiano na IMO na mchango wake katika kuimarisha nafasi ya Tanzania kama taifa muhimu katika eneo la Bahari ya Hindi, akisisitiza nafasi ya Tanzania katika jitihada za utunzaji wa rasilimali bahari ili iendelee kuwa na mchango kwenye uchumi ikiwemo kupitia bandari ambazo zimekuwa na mchango mkubwa katika biashara ya kikanda na ya kimataifa.

“Tunaitambua IMO kama mshirika muhimu katika kujenga uwezo wa Tanzania kwenye masuala ya bahari na kusaidia juhudi zetu za kuboresha sekta hii kwa kuzingatia viwango vya kimataifa,” alisema Mhe. Waziri Kombo.

Naye  Katibu Mkuu wa IMO Domínguez aliipongeza Tanzania kwa ushiriki wake wa dhati katika programu na miradi ya IMO na kuahidi kuendelea kushirikiana katika maeneo ya mafunzo, fursa za ajira, utawala wa masuala ya bahari, mchakato wa kupunguza hewa ukaa kwenye usafiri wa meli, na mapambano dhidi ya uvuvi haramu, usioripotiwa na usiodhibitiwa (IUU).

“Tanzania ni mshirika muhimu wa masuala ya bahari, na tumejipanga kushirikiana kwa karibu na Serikali kuhakikisha sekta ya bandari na usafirishaji inaendelea kukua kwa njia endelevu sambamba na kanuni za kimataifa za usalama na mazingira,” alisema.

Mazungumzo hayo pia yaligusia fursa za kuimarisha msaada wa kiufundi kwa mabaharia wa Kitanzania, kuongeza uwezo wa taasisi za masuala ya bahari, na kulinganisha mkakati wa Tanzania wa Uchumi wa Buluu na ajenda ya IMO ya mabadiliko ya kijani na kidijitali katika sekta ya usafirishaji majini.

Waziri Kombo yuko nchini Uingereza kwa ziara rasmi ambayo pamoja na masuala mengine inalenga kuendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria na kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Uingereza.