Oct 15, 2025

DKT NATU AKUTANA NA WAKURUGENZI WA IMF JIJINI WASHINGTON

 


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, DKT. Natu El-maamry Mwamba (kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa( IMF) , Bw. Adran Ubisse, baada ya kikao chao kilichofanyika Makao Makuu ya Taasisi hiyo, Jijini Washington D.C, nchini Marekani, ambapo katika mazungumzo yao Bw. Ubisse aliipongeza Tanzania kwa kuwa na rekodi nzuri ya utekelezaji wa miradi kwa kutumia vizuri fedha inazokopa.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, DKT. Natu El-maamry Mwamba (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika wa Shirika la Fedha la Kimataifa( IMF) , Bw. Adran Ubisse ( wa pili kulia), Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil (wa pili kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Kanza (wa kwanza kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao kilichofanyika makao makuu ya IMF, jijini Washington D.C, nchini Marekani.


Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, DKT. Natu El-maamry Mwamba (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) anayesimamia Idara ya Afrika, Bw. Abebe Selassie (wa pili kulia), Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu-Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil (wa pili kushoto) na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Dkt. Elsie Kanza (wa kwanza kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao kilichofanyika makao makuu ya IMF, jijini Washington D.C, nchini Marekani.