Na ili kufanikisha zoezi hilo, Jeshi
la Wananchi (JWTZ) limeombwa kushiriki huku mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam akizuia mikutano yoyote ambayo itaonekana haina tija.
Chadema ilikuwa imepanga kuzindua
operesheni iliyoibatiza jina la Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania
(Ukuta), kwa kufanya mikutano na maandamano kote nchini, lakini
ikatangaza kuahirisha juzi ikieleza kuwa imezingatia ushauri kutoka kwa
viongozi wa dini, taasisi na watu mashuhuri.
“Nimezungumza na watu wa hali ya
hewa, wameniambia tukianza mapema miti hii haitakufa. Siku ya Oktoba
Mosi kila mtu atakuwa na mti wake, tutawaarifu kupitia wakuu wa wilaya
miti itapatikana wapi baada ya taratibu zake kukamilika,” alisema Makonda jana mbele ya Rais Magufuli kwenye mkutano wa 14 wa wahandisi kwenye ukumbi wa Mlimani City.
Makonda alisema siku hiyo vikosi vya
ulinzi na usalama vitashiriki kupanda miti na kumuomba Rais amsaidie na
amvumilie ili atende kazi yake ya kuhakikisha mkoa wa Dar es Salaam
unakuwa na amani sambamba na kufanikisha kutekeleza mpango huo wa
upandaji miti.
Aidha, makonda alipiga marufuku kufanyika kwa mikutano au maandamano
yoyote isipokuwa mikutano itakayokuwa inajadili shughuli za maendeleo.
“Watakaopewa kibali ni wale
wanaojadili maendeleo, lakini si wapigakelele. Mikutano kama hii (ya
wahandisi) inayojadili masuala muhimu kabisa kwa maendeleo ya nchi,
itaruhusiwa bila shaka yoyote.”
Makonda alisema kampeni hiyo
itawahusisha pia wananchi, viongozi wa dini na kamati nzima ya ulinzi na
usalama ya mkoa wa Dar es Salaam na kwamba jumla ya miti milioni 4
inatarajiwa kupandwa siku hiyo.
Alisema ameamua kushirikisha vyombo
vya ulinzi na usalama kwa sababu ni watiifu na wazalendo kwa Taifa
wakati kada nyingine zimejielekeza kwenye siasa.
Hata hivyo, Rais hakuzungumzia maombi hayo zaidi ya kusema kuwa Makonda naye amekuwa mhandisi kutokana na kutoa maelekezo.
Kabla ya Makonda kutangaza Oktoba Mosi
kuwa siku ya kupanda miti, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema
wamekutana na viongozi wa dini zaidi ya mara moja kwa ajili ya kupata
maoni na ushauri kuhusu maandamano yao, ambayo Jeshi la Polisi
liliyapiga marufuku kwa maelezo kuwa yalikuwa na viashiria vya kuvunja
amani.
Baadaye JWTZ ilisema ingeadhimisha
kuzaliwa kwa jeshi hilo kwa askari wake kufanya mazoezi na kuonyesha
silaha zao za angani na nchi kavu, kufanya usafi mitaani na kujitolea
damu, huku likibainisha kuwa linaamini hakungekuwa na maandamano yoyote
kwa kuwa yameshazuiwa.
Katika kuadhimisha miaka 52 ya JWTZ
jana, Makonda alishiriki kufanya usafi na askari hao katika kambi ya
Lugalo iliyopo wilayani Kinondoni.
Makonda aliambatana na kamati ya amani ya viongozi wa dini wa Dar es Salaam, ikiongozwa na mwenyekiti wake Alhadi Mussa Salum.
Makonda aliitaja barabara ya Mwenge
–Ubungo kuwa ni miongoni mwa barabara zitakazopandwa miti siku hiyo na
watashirikiana na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads)