Satelaiti hiyo iliharibiwa katika mlipuko uliotokea eneo la Cape Canaveral jimbo la Florida, Marekani siku ya Alhamisi.
Satelaiti hiyo kwa jina Amos-Six ilikuwa
imebebwa na roketi ya Falcon Nine ambayo ililipuka ilipokuwa ikifanyiwa
majaribio ya kujiandaa kwa safari ya siku ya Jumamosi.
Bw Zuckerberg, ambaye yumo ziarani Afrika, amesema “nimesikitishwa sana” kusikia kwamba satelaiti hiyo iliharibiwa.
“Tutaendelea kujitolea katika lengo
lengo la kufikisha huduma ya mtandao kwa kila mtu na tutatia bidii hadi
kila mtu apate nafasi na manufaa ambayo yangetokana na satelaiti hii,”
aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa kulipuka
kwa roketi hiyo ni pigo kubwa kwa mwanabiashara Elon Musk ambaye ni
mmiliki wa kampuni ya kuunda roketi ya Space X.
Afisa mmoja wa masuala ya anga za juu wa
Israeli amesema satelaiti ya Amos-6 inakadiriwa kuwa na thamani ya
$200m (£150m) na ilimilikiwa na kampuni kwa jina Spacecom, was a major
blow to the industry.
“Hili ni pigo kubwa sana ambalo huenda
ikaathiri mustakabali wa sekta ya satelaiti na huenda ikahitaji kupigwa
jeki (kifedha),” alisema mwenyekiti wa taasisi ya masuala ya anga za juu
ya Israel, Isaac Ben-Israel.