
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 15 Septemba, 2016
amemteua Mhandisi Emmanuel Korosso kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ndege
Tanzania (ATCL).
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa
Mhandisi Emmanuel Korosso unaanza mara moja.Mhandisi Emmanuel
Korosso anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Salim Msoma ambaye alimaliza muda
wake.
Wakati
huo huo, Rais Magufuli amemteua Mhandisi Ladislaus
Ernest Matindi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).
Kabla ya uteuzi
huu Mhandisi Ladislaus Ernest Matindi alikuwa Mkurugenzi katika Shirika linaloshughulikia
masuala ya usafiri wa anga Barani Afrika (EGNOS-Africa Joint Programme Office)
lenye makao yake nchini Senegal.
Uteuzi huu unaanza
mara moja.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es
Salaam
15
Septemba, 2016