Daktari wake Lisa Bardack amesema kuwa
Bi Clinton amekutwa na ugonjwa huo tokea Ijumaa na kuongeza kuwa,
Clinton aliongezeka joto na kuishiwa na maji mwilini katika tukio hilo
la kuwakumbuka wahanga wa shambulio la Al-Qaeda lililotokea Tuesday,
Septemba 11, 2001.
Maelfu ya watu walikusanyika eneo la
Ground Zero huko New York wakiadhimisha miaka miaka 15 tangu kundi la
kigaidi la Al-Qaeda lililokuwa linaongozwa na Osama Bin Laden, kwa
kuipua majengo mawili marefu zaidi duniani ambapo ni Makao Makuu ya
Jeshi la Marekani, Pentagon na kuuwa watu 2,996 huku wakijeruhiwa watu
6,000 na kusababisha hasara ya jumla ya dola trilioni 3.
Baada ya hali hiyo kuokea ghafla,
Clinton alilazimika kuondoka mapema, picha zilizowekwa mtandaoni
zinamuonesha akisaidiwa na msaidizi wake, huku akitaka kuanguka
alipokaribia kwenye gari, lakini baadae bi clinton alitokea kwenye
nyumba ya mwanae na kuwaambia waandishi wa habari kuwa anajisikia
vizuri.
Awali mgombea Urais kupitia chama cha Republican Donald Trump alionesha wasiwasi juu ya afya ya hasimu wake.
Katika shughuli hiyo majina karibu 3000 ya wahanga wa shambulizi la Septemba 11 yalisomwa.