
BUKOBA: September 10, 2016 lilitokea
tetemeko la ardhi Kagera kanda ya ziwa Tanzania lenye kipimo cha ritcha
5.7 na kusababisha vifo vya watu 16 na wengine zaidi ya 120 kujeruhiwa
ambapo ndani ya saa 24 baadae (September 11 saa tano kasoro usiku)
likatokea tena tetemeko jingine na kuacha tahauki kwa wakazi wa Bukoba.

Tetemeko hilo la pili ambalo ni dogo
halijaripotiwa kusababisha majeruhi au vifo mpaka usiku wa saa nane
lakini limeleta hofu kwa wakazi wa Bukoba ambao baadhi wameamua kutoa
magodoro nje ya nyumba zao na kulala kwa kuhofia tetemeko linaweza
kutokea tena usiku na kuwakuta ndani ya nyumba zao.
