Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Nkoarisambu iliyopo wilayani Meru mkoani Arusha.
Wilaya ya Arumeru Mkoani
Arusha imebaini kuwepo kwa wanafunzi hewa 10,636 katika shule za msingi
na sekondari zilizopo katika wilaya hiyo ambao wanaigharimu serikali
zaidi ya shilingi milioni 100. Mkuu
wa wilaya hiyo Alexender Mnyiti amebainisha hayo katika kikao cha
watendaji wa halmashauri, wataalam na watumishi wa umma, ambapo amesema
idadi hiyo imebainika baada ya uchunguzi katika shule 94 za msingi na
sekondari zilizopo katika wilaya hiyo.
Mkuu huyo wa Wilaya amemtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha anawafukuza kazi wakuu wa shule hizo na kuteua wakuu wapya ili kurejesha nidhamu ya utumishi wa umma na kwa serikali.
Aidha ametaka hatua za kinidhamu zichukuliwe kwa watumishi wote watakaobainika kuhusika na uwepo wa wanafunzi hewa kwa kosa la udanganyifu.