Vipande vya sigara vilivyotumika
Wavutaji sigara nchini Kenya watalipa nyongeza ya kodi ya shilingi
milioni 650 za nchi hiyo kwa mwaka kufuatia kuridhiwa kwa sheria
inayolenga kukatisha tamaa tabia ya uvutaji sigara. Malipo
hayo mapya ya kodi yataongeza gharama za sigara za aina mbalimbali
ambazo zipo juu kiasi kwa sasa ambapo sigara bei ya kawaida inauzwa
shilingi 15 za Kenya kwa moja na pakiti ni shilingi 300.
Kodi hiyo mpya ya sigara inalenga kukatwa kwa asilimia mbili ya mauzo ya sigara Kenya kwa mwaka yanayofikia shilingi bilioni 32 za nchi hiyo.
Kodi hiyo mpya ya sigara inalenga kukatwa kwa asilimia mbili ya mauzo ya sigara Kenya kwa mwaka yanayofikia shilingi bilioni 32 za nchi hiyo.