Aliyekuwa Mkuu wa tume ya kupambana na rushwa Kenya (EACC) Philip Kinisu.
Mkuu wa tume ya kupambana na
rushwa nchini Kenya (EACC) Philip Kinisu, amejiuzulu ikiwa ni siku moja
baada ya kamati ya bunge kupendekeza afutwe kazi kwa sababu ya
muingiliano ya maslahi.
Lakini kampuni ambayo inamilikiwa na Kinisu inadaiwa kushiriki katika shughuli za kibiashara na NYS.
Wabunge walikuwa wamemuomba Rais Uhuru Kenyatta aunde jopo la kumchunguza, na kuamua iwapo anafaa kufutwa kazi.
Kinisu, ambaye ni mwenyekiti wa zamani ya kampuni ya wahasibu ya PwC Afrika aliteuliwa kuongoza tume hiyo Novemba mwaka jana.