- KUKAMATWA KWA BASTOLA AINA YA BWOWNING NA RISASI 06
Katika tukio la kwanza
mnamo tarehe 22.08.2016 03:45 hrs huko maeneo ya Mabibo Loyola, kata ya
Mabibo (W) Magomeni kikundi cha Ulinzi shirikishi wa eneo hilo wakiwa
kazini waliona kundi la watu kati ya watu watatu hadi wanne wakiwa
wanatembea.
Baada ya kuwaona waliwatilia shaka na
kuwasimamisha iliwaweze kuwahoji. Hata hivyo katika mahojiano watuhumiwa
wengine walifanikiwa kukimbia ambapo mtuhumiwa mmoja mwanaume
asiyefahamika anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka (20 – 25)
alikamatwa.
Baada ya mtu huyo kukamatwa alianza kuwatishia kuwa atawaua huku akitamka maneno ya kiislam akisema ”Taqbir” na “Allah Huaqbar “ ghafla mtu huyo aliingiza mkono mfukoni na kutoaa kitambaa cha kufuta jasho na kukitupa chini ambapo bomu
lililipuka. Kuona hivyo ulinzi shirikishi walikimbia na mtu huyo kuanza
kukimbia huku akiwa na begi mgongoni. Hata hivyo mmoja kati ya hao
ulinzi shirikishi alimpiga mtuhumiwa huyo rungu kichwani eneo la
kisogoni, pamoja na kupigwa rungu kichwani mtu huyo aliendelea kukimbia
na alitupa begi chini na kuendelea kukimbia. Ulinzi shirikishi nao
waliendelea kumkimbiza na kufanikiwa kumkamata ambapo wananchi
walijitokeza na kumpiga hadi kufa kisha kumchoma moto. Askari polisi
baada ya kupata taarifa hizo, walifika eneo la tukio ambapo ulifanyika
upekuzi katika begi hilo na kukutwa magazine 10 za SMG zikiwa na jumla
ya risasi 300.
Hadi sasa askari wapo eneo la tukio
wakifanya upekuzi katika nyumba mbalimbali kuwatafuta watuhumiwa wengine
ambao inasadikiwa bado wapo eneo hilo. Msako mkali unaendelea
kuwatafuta watuhumiwa hao waliokimbia.
KUUAWA KWA MAJAMBAZI WAWILI KATIKA MAJIBIZANO YA ANA KWA ANA
Katika tukio lingine
tarehe 21.08.2016, saa 21:30hrs usiku huko Tandika Mtaa wa Chiwanda
nyumba no. 08 Mkoa wa Temeke, Kikosi Maalum cha Kupambana na Ujambazi wa
kutumia silaha cha Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam kilifanikiwa
kuwaua majambazi wawili katika majibizano ya risasi ya ana kwa ana.
Tukio hilo lilitokea katika maeneo hayo
ambapo askari walipata taarifa kutoka kwa msiri kuwa kuna kundi la
majambazi wanataka kuvamia nyumba hiyo.
Mara baada ya kupokea taarifa hizo
Askari walifika eneo la nyumba hiyo kabla ya majambazi hao hawajaanza
kupora ambao idadi yao walikuwa watano wakiwa na pikipiki mbili ambazo
hazikusomeka namba.
Baada ya majambazi hayo kugundua kuwa
wanafuatiliwa majambazi hayo walianza kuwafyatulia askari risasi ambazo
hazikuleta madhara, ndipo askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwapiga
risasi majambazi wawili wanaume umri kati ya miaka (25 – 30), ambao
walifariki dunia papo hapo na wengine watatu walifanikiwa kutoroka.
Katika upekuzi mmoja wa majambazi hao
alikutwa na bastola moja aina ya Browining ikiwa na risasi 06 namba zake
zikiwa zimefutwa. Jitihada za kuwatafuta majambazi waliokimbia
unafanyika na upelelezi unaendelea.
KUPATIKANA KWA SARE AINA YA FULANA ZENYE MANENO YA UCHOCHEZI ZIKIWA NA ALAMA YA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dsm mnamo
tarehe 20/08/2016 majira ya saa 12:00 jioni lilipata taarifa toka kwa
raia wema kuwa maeneo ya mtaa wa Ufipa Kinondoni kuna duka linauza flana
rangi mbalimbali zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ rangi nyeupe idadi yake 28, rangi nyekundu fulana 18 zenye maneno ‘UKUTA’ fulana 6 za Kakhi zenye maneno ‘’UKUTA’ Na fulana zingine rangi nyeusi 23 zenye maneno ’’UKUTA’’.
Aidha Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa aitwaye YORAM SETHY MBYELLAH
miaka 42, mfanyabiashara, mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo
dukani kwake. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na baada ya upelelezi
kukamilika atafikishwa mahakamani.
KUKAMATWA KWA MTUHUMIWA KWA KOSA LA WIZI WA GARI
Mnamo tarehe 09.08.2016 saa 18:00hrs
jioni huko Masasi Mjini kwenye gereji ya magari, Kikosi Maalum cha
Kupambana na wizi wa Magari cha Polisi Kanda maalum cha Dar Es salaam
kimefanikiwa kumkamata mtuhumiwa OMARY GILLIAD OMARY (35) kazi dereva
kwa wizi wa gari. Mtuhumiwa alikamatwa kwa wizi wa gari No: T.612 AUJ
aina ya Toyota Hiace mali ya mlalamikaji KAISARI MWALIMU YUSUFU (26)
Mfanyabiashara mkazi wa Sinza.
Gari hilo iliyoibiwa tarehe 25.06.2016
likiwa limeegeshwa nyumbani kwa mlalamikaji maeneo ya Sinza ambapo
mtuhumiwa alichukua gari hilo kwa nia ya kufanya kazi.
Baada ya mtuhumiwa kupewa gari hilo
aliipeleka mafichoni Masasi Mjini mkoani Mtwara ambapo Kikosi cha
Kupambana na Wizi wa Magari Cha Polisi Kanda Maalum ya Dar Es salaam
kilifanya ufuatiliaji na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa pamoja na
kielelezo gari. Mtuhumiwa anahojiwa na upelelezi utakapokamilika
atapelekwa mahakamani kujibu shutma inayomkabili dhidi yake.
KINARA MWIZI WA VIFAA VYA MAGARI AKAMATWA AKIWA NA VIFAA MBALIMBALI VYA MAGARI
Kikosi maalum cha kupambana na wizi wa
magari cha Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam kimefanikiwa kumkamata
mtuhumiwa hatari anayejihusisha na wizi wa magari na viafaa vyake.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa tarehe 01/08/2016 majira ya saa 08:30 usiku,
maeneo ya amani mtaa wa kongo askari wakiwa doria walifanikiwa
kumkamata mtuhumiwa mmoja aitwaye SALUMU S/O ISSA @HASSANI (43) Mkazi wa mbagala akiwa na (1).SIDE MIRROR 12 (2). SITE MIRROR 11(3) CAMP BAMPA 24 (3).PLATE SIDE MIRROR 44 (4) VITASA28 (5).SIDE LAMP 11 (6).INDICATOR 17
vifaa hivyo Vyote vikiwa ni mali za wizi akiwa ameviiba na baada ya
kumhoji alikiri kuhusika na wizi huo. Mtuhumiwa huyo atapelekwa
mahakamani wakati wowote upelelezi utakapokamilika.
TAARIFA YA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KANDA MAALUM YA D’SALAAM KUANZIA TAREHE 21.08.2016 HADI TAREHE 22.08.2016.
Taarifa ya Kikosi cha Usalama
barabarani Kanda Maalum ya D’salaam ya ukamataji wa makosa ya Usalama
Barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 21.08.2016 hadi tarehe
22.08.2016 ni kama ifuatavyo:-
- Idadi ya magari yaliyokamatwa 5,346
- Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa 216
- Daladala zilizokamatwa 1,121
- Magari mengine (binafsi na malori) 225
- Jumla ya Makosa yaliyokamatwa 20,562
Jumla ya fedha za Tozo zilizopatikana TSH 161,750,000/=
S.N.SIRRO – CP
KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM