
Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamidu.
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wanatarajia kufanya
maandamano ya Amani nchi nzima Agosti 31 kwa ajili ya kueleza utendaji
kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa Watanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Kaimu
Katibu Mkuu wa Umoja huo, Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa
wameshamwandikia barua mkuu wa jeshi la Polisi kwa ajili ya kupata
ulinzi siku hiyo
Amesema kuwa wasipopata ulinzi watafanya kwa kujilinda wenyewe
ikiwa ni lengo la kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya utendaji kazi wa
Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Shaka amesema kuwa Rais Dk.John Pombe Magufuli amefanya watendaji
kuwa na utii pamoja na maadili katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha amesema kuwa katika maandamano hayo wanaawalika na vijana wa
vyama vingine kushiriki kwa lengo moja tuu,la kuunga mkono utendaji wa
Rais Dkt.John Pombe Magufuli