Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiongozana na baadhi ya viongozi wa Wizara
na Uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili katika makabidhiano ya Uwanja wa
Uhuru leo 22 Agosti 2016.
Mhandisi Mshauri Bw Aloyce
Moshi(Kulia) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye(katikati) kuhusu
matengenezo yaliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru , kushoto kwake ni katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akijadiliana jambo na katibu Mkuu wa Wizara
ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel wakati alipokuwa
akikagua matengenezo ya Uwanja wa Uhuru leo Agosti 22 , 2016 kulia ni Mhandisi
Mshauri Bw Aloyce Moshi
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akiangalia eneo ambalo limetengwa
kwa ajili ya ujenzi wa ofisi
mbalimbali kulia ni katibu Mkuu wa Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel na kushoto ni Mhandisi Mshauri Bw Aloyce
Moshi.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wakati wa
makabidhiano ya Uwanja wa Uhuru leo Agosti 22,2016 .
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akiangalia nyasi za Uwanja wa Uhuru mara
baada ya kukabidhiwa uwanaja huo baada ya matengenezo leo Agosti 22,2016 .
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye(katikati)
akijadiliana jambo na katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia) wakati alipokuwa akikagua
matengenezo ya Uwanja wa Uhuru leo Agosti 22 , 2016 kulia ni Mhandisi Mshauri
Bw Aloyce Moshi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akiweka saini makabidhano
ya Uwanja wa Uhuru kati ya Serikali na
Kampuni ya BCEG ya China leo Agosti 22,2016.
Meneja wa kampuni BCEG Bw. Cheng Longhai akiweka saini
makabidhano ya Uwanja wa Uhuru kati ya
Serikali na Kampuni yake ya BCEG leo Agosti
22,2016.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(kulia) akibadilishana hati
za makabidhiano ya Uwanja wa Uhuru mara baada ya kumalizika kwa matengenezo leo
Agosti 22,2016.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel(kulia) akionesha hati ya makabidhiano ya Uwanja wa Uhuru kwa
waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa matengenezo ya uwanja huo leo Agosti
22,2016 (katikati ) ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape
Moses Nnauye.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza na waandishi wa habari na wadau wa michezo
mara baada ya makabidhiano ya Uwanja wa Uhuru leo Agosti 22,2016.
Muonekano wa Uwanja wa
Uhuru mara baada ya matengenezo.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM
Vyama
vya michezo nchini vimeshauriwa kujenga ofisi zao ndani ya uwanja wa Uhuru
kuepukana na gharama za kukodi ofisi katika maeneo mengine.
Ushauri
huo umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye wakati akipokea Uwanja wa Uhuru uliokuwa
unafanyiwa matengenezo na kampuni ya CBG.
Mhe.
Nape Moses Nnauye amesema kuwa mpaka sasa michoro kwa ajili ya majengo ndani ya
Uwanja huo ipo tayari na vyama vya michezo vinakaribishwa kuanza kujenga ofisi
zao.
“Kama
kuna vyama vya michezo vyenye uwezo binafsi au kama wanaweza kupata ufadhili wa
kuja kujenga ofisi zao humu michoro ipo tayari na eneo lipo tayari ata kesho waje
wajenge ” alisema Mhe. Nape.
Mhe.
Nape amesisitiza kuwa zoezi hili litaratibiwa na Serikali moja kwa moja na kutoa
nafasi kwa vyama vyenye uwezo kujitokeza na kuchangamkia fursa hiyo ambapo ramani,michoro na eneo lipo tayari kwa ajili
ya zoezi hilo.
Aidha
Serikali imewaalika wadau mbalimbali kuwekeza katika michezo kwa kujenga
miundombinu itakayosaidia kukuza vipaji kwa wanamichezo mbalimbali na kusukuma
gurudumu la maendeleo ya sekta ya
michezo nchini.
Kwa
upande wake katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof
Elisante Ole Gabriel amevishauri vyama vya michezo nchini kuchangamkia fursa
iliyotolewa na Serikali ya kujenga ofisi za vyama vyao ndani ya Uwanja wa Uhuru
na kushauri wadau wa michezo kuwekeza zaidi katika michezo hasa kwa vijana.
“
Wadau kimbilieni fursa ndio hii ya kuwekeza katika michezo pamoja na vyama vya
michezo kujenga ofisi zao ndani ya Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya maendeleo yao
na michezo nchini” alisema Prof Gabriel.