Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande,
alisema jana kuwa mkandarasi aliyekabidhiwa kazi ya kukarabati majengo
hayo yaliyopo katika Shule Kuu ya Sheria, pembeni mwa kituo cha mabasi
cha Simu 2000, Ubungo Dar es Salaam, yako katika hatua za mwisho za
ukarabati.
Akizungumza katika viwanja vya
Karimjee baada ya kuapisha mawakili wapya 623 wa Mahakama Kuu, Jaji
Chande alisema tayari Bunge limeshapitisha muswada wa sheria ya
uanzishwaji wa mahakama hiyo.
Alisema kwa sasa muswada huo
utawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya
kuusaini ili uwe sheria, kisha sheria hiyo itatangazwa katika gazeti la
Serikali ili kuruhusu shughuli za mahakama hiyo kuanza.
Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama iko
tayari kuendesha Divisheni hiyo ya Mahakama na baada ya kukabidhiwa
majengo hayo, wataanza kutoa semina kwa majaji na watumishi wengine wa
mahakama hiyo, kuhusu divisheni hiyo itakavyoendesha shughuli zake.
Aliweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna kesi hata moja iliyokwishatambuliwa kwamba itashughulikiwa na mahakama hiyo