KAMPUNI
ya teknolojia ya Apple nchini Marekani inadaiwa kutaka kuchukua umiliki
wa huduma ya kusikiliza muziki ya moja kwa moja kutoka Kapuni ya Tidal
inayomilikiwa na mwanamuziki maarufu duniani Jay Z .
Apple imeripotiwa kwamba inataka
kuinunua Tidal kutokana na ushirikiano wake na wanamuzika bingwa kama
vile Kanye West na Madonna ambao wanafanya kazi za kimuziki na Tidal.
Jarida
la Wall Street limechapisha taarifa kuwa mazungumzo yameanza kati ya
wamiliki wa makampuni hayo mawili na huenda makubaliano yakafikiwa hivi
karibuni na hatimaye biashara kufanyika. Wakati taarifa hizo za Wall
Street zikisambaa, Msemaji wa Tidal amekana kufanya mazungumzo na Apple.
Jay Z alizindua huduma hiyo Machi 2015
kama mpinzani wa Spotify baada ya kununua Kampuni ya kiteknolojia ya
Sweden, Aspiro ambayo ilikuwa ikiimiliki Tidal kwa takriban dola milioni
56.
Wadeau wengine kwenye Kampuni ya Tidal mbali na Jay Z ni mkewe, Beyonce, rapa Kanye West na Alicia Keys.