KUTOKANA na kuongezeka kwa
vitendo vinavyoashiria kuwepo kwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya
jinsia moja, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza
operesheni ya kuwasaka wanaume wanaojihusisha na tabia hiyo mbovu ya
‘mashoga’ jijini humo ilihali wakijua ni kinyume cha sheria za nchi.
Makonda amesema vitendo hivyo vimeanza
kuongezeka jijini humo na lengo lake ni kuwaokoa watoto wasiige mambo
hayo yanayoonekana kukua kwa kasi.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema, “hili ni tatizo linalokua kwa kasi sitaruhusu liendelee katika mkoa wangu, nitawasaka popote walipo”.
“Hata hapa bandari wanaweza kuwapo mashoga wafichueni, mkiona mtu ana tabia za ajabu ajabu mfichueni, tutashughulika nao”.