WANASAYANSI maarufu kutoka
Taasisi moja kubwa ya Sayansi nchini Uingereza wametoa ripoti ya utafiti
walioufanya ikithibitisha kwamba, Rais wa Zimbabwe, Komrade Robert
Mugabe amegundulika kuwa na vinasaba (genes) ambavyo vitamfanya aishi
milele (asife).
Robert Mugabemiaka ya 1980.
Utafiti huo wa siri unaongozwa na
Daktari Irvin Koch umegharimu mabilioni ya fedha na kugundua pia kwamba
Bob Robert mwenye miaka 92 sasa haweki dawa kichwani (SUPER BLACK) wala
hajawahi kukata nywele zake licha ya kutojihangaisha na kula vyakula vya
mimea (veggies) ama kwenda gym kufanya mazoezi.
Katika tafiti hiyo, Wanasayansi hao
walichukua sampuli mbalimbali kutoka kwa Bob ikiwemo damu yake, nguo
zake, miswaki aliyokuwa akitumia, na hata chanuo kwa miongo kadhaa na
kugundua kuwa hakuna hata chembe ya umauti kwa Mugabe.
Baadhi ya watu wameanza kuamini kuamini
tafiti hizo baada ya kugundua kutoka kwenye picha za Mugabe akiendelea
kupeta katika muonekano huohuo huku akiwa mwenye siha ya haja kwa miaka
mingi sasa.
Mpinzani wake mkuu kwenye siasa za
Zimbabwe ambaye ni Kongozi wa Chama cha MDC, Morgan Tsvangirai (ama kwa
kuguswa kwamba ausahau uraisi) amejibu kwa kejeli kwamba ‘Mugabe ni
makusanyo ya nyama na mifupa kama hayawani wengine wote’ na kwamba kila
nafsi itaonja mauti (Kul nafsi dhalika lmaut).
Inasemekana kwamba utafiti huo unaendelea mpaka mwaka 2018 ndipo utakamilika.
Source: Newssa/Mzansi SatireZimbabwe News Day===http://bit.ly/1rlaUBX