Jun 13, 2016

Baada ya Sintofahamu… Zitto Kabwe ajitokeza

zitto
Kiongozi Mkuu wa ACT Zitto Kabwe amejitokeza leo kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam baada ya taarifa kutolewa jana na chama chake kuwa hawajui alipo tangu juzi Jumamosi juni 11.
Akizungumza na wanahabari leo baada ya kujitokeza, Mh. Zitto Kabwe amesema kuwa hatishiki na vitisho vinavyotolewa na Jeshi la Polisi nakwamba amekusudia kufanya kongamano la kujadili bajeti kesho Makao Makuu ya Chama hicho huku akiitaka jeshi la Polisi kuacha kumvizia na badala yake limkamate kwa kufuata Sheria