Fundi nguo maarufu mjini hapa,
Bahati Anthony aliyedai ni ‘wakala’ wa jamii ya siri inayohusishwa na
utajiri wa ghafla na imani za kishetani ya Freemason, amenusa kifo baada
ya kunaswa kwa utapeli kwa wakala wa mitandao yasimu inayotoa huduma ya
kuweka na kutoa fedha.
Tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki
iliyopita maeneo ya Masika katikati ya Mji wa Morogoro kwenye duka la
wakala aitwaye Gelasi Assenga ambapo jamaa huyo alijikuta akiloa damu
chapachapa.
Akisimulia tukio hilo, Assenga alikuwa na haya ya kusema: “Jana huyu jamaa alikuja hapa akatuma shilingi 15, leo amekuja ameniambia nitume laki tatu kwenye namba ileile aliyonipa jana.
Akisimulia tukio hilo, Assenga alikuwa na haya ya kusema: “Jana huyu jamaa alikuja hapa akatuma shilingi 15, leo amekuja ameniambia nitume laki tatu kwenye namba ileile aliyonipa jana.
“Nimemwambia anipe fedha zangu, anasema haijaingia, nikaamua kumpekua kwenye begi nikakuta mshumaa.”
“Wakati napekuwa ndipo akaanza kukimbia. Nilipoona nitapoteza fedha zangu, nikaona nimwitie mwizi ndipo watu wakamkamata na kumshushia kichapo.
“Nilipoona
wanataka kumuua, nilikodi bodaboda na kumpeleka polisi ambako baada
Inaendelea Uk.4 Kutoka Moro ya kuhojiwa alisema yeye siyo mwizi bali
alielekezwa kufanya hivyo na kiongozi wa Freemason.
“Hata hivyo, polisi walimwamuru kurudisha fedha zangu ambapo aliwapigia simu ndugu zake kutoka Kigoma ambao walidai kuwa watanitumia fedha yangu ndipo aachiwe huru.”
“Hata hivyo, polisi walimwamuru kurudisha fedha zangu ambapo aliwapigia simu ndugu zake kutoka Kigoma ambao walidai kuwa watanitumia fedha yangu ndipo aachiwe huru.”
“Baadaye waliniambia ninunue begi jipya
ndani yake niweke mshumaa na udi kisha niende palepale kwa wakala wa
jana yake niwatumie shilingi laki tatu. “Niliwaambia fedha hiyo sina,
wakaniambia nimwambie wakala anitumie tu baada ya dakika 10 begi langu
litajaa fedha lakini haikuwa hivyo ndiyo maana ssenga akaniitia mwizi
nikapigwa.”
Kumekuwa na utapeli wa aina hiyo mkoani hapa hivyo Wikienda linawataka wasomaji wake kuwa macho ili wasilizwe.
Kumekuwa na utapeli wa aina hiyo mkoani hapa hivyo Wikienda linawataka wasomaji wake kuwa macho ili wasilizwe.