Waziri
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (mbele) akiongoza kikao
kati yake na kampuni inayojishughulisha na usambazaji wa vifaa na
teknolojia katika utafutaji wa mafuta na gesi ya Schlumberger. Pia kikao hicho kilihusisha watendaji kutoka Wizara hiyo pamoja na taasisi zake likiwemo Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Meneja Masoko kutoka kampuni ya Schlumberger, Abdul Adeshina (hayupo pichani) katika kikao hicho.
Meneja
Masoko kutoka kampuni ya Schlumberger, Abdul Adeshina akielezea
shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kusambaza vifaa
na teknolojia kwa ajili ya utafiti wa mafuta na gesi nchini.
Na Greyson Mwase, Dar es Salaam
WAZIRI
wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ametaka makampuni
yanayojishughulisha na shughuli za utafutaji na uchimbaji wa gesi na
mafuta nchini kuongeza kasi ya utafiti kwa kutumia teknolojia ya kisasa
ili sekta ya gesi na mafuta iweze kukua na kuchangia ukuaji wa uchumi
wa nchi.
Profesa
Muhongo alitoa kauli hiyo alipokutana na kampuni inayojishughulisha na
usambazaji wa vifaa na teknolojia katika utafutaji wa mafuta na gesi
ya Schlumberger yenye makazi yake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
kujadili utendaji kazi wa kampuni hiyo.
Kikao
hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam kilihusisha watendaji kutoka
Wizara hiyo pamoja na taasisi zake likiwemo Shirika la Maendeleo ya
Petroli Nchini (TPDC), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Wakala wa
Nishati Vijijini (REA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na
Maji (EWURA).
Alisema Tanzania
kwa sasa ina utajiri mkubwa wa rasilimali ya gesi ambayo itachochea
katika ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia umeme wa uhakika utakaotumika
katika viwanda na kuongeza ajira kwa vijana wa kitanzania.
Aliendelea
kusema kuwa ili sekta ya gesi na mafuta iweze kuwa na mchango katika
ukuaji wa uchumi wa nchi, Tanzania inahitaji wawekezaji watakaowekeza
kwa kasi kwa kutumia teknolojia ya kisasa.
Alisisitiza
kuwa serikali ipo tayari kushirikiana na mwekezaji yeyote mwenye nia
ya kuwekeza kwenye sekta ya gesi na mafuta kwa kutumia teknolojia ya
kisasa.
“
Kama serikali tumedhamiria kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa miongoni
mwa nchi zenye utajiri unaotokana na rasilimali za gesi na mafuta,
hivyo tunapenda kushirikiana na wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali
ndani na nje ya nchi kwa kutumia teknolojia ya kisasa,”
alisema Profesa Muhongo
Profesa
Muhongo aliihakikishia kampuni ya Schlumberger kuwa serikali itafanya
kazi kwa karibu nayo na kutoa ushirikiano wowote utakaohitajika ili
sekta ya gesi na mafuta iweze kukua kwa kasi na kuchochea ukuaji wa
uchumi wa nchi.
Awali
akizungumza katika kikao hicho Meneja Masoko kutoka kampuni ya
Schlumberger, Abdul Adeshina alisema kampuni yake imekuwa
imekuwa ikitoa mafunzo kwa wafanyakazi wa kitanzania asilimia 80
wanaofanya kazi katika kampuni hiyo.
Aliongeza
kuwa kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana kwa karibu na Shirika la
Maendeleo ya Petroli Nchini (TPDC) katika shughuli za utafiti wa mafuta
na gesi nchini na kusisitiza kuwa kampuni hiyo ipo tayari kutumia
teknolojia na vifaa vyake katika kuboresha shughuli za utafutaji wa
mafuta na gesi nchini.