Pichani viongozi wa wilaya ya Shinyanga,wazazi na maafisa kutoka Lions Club International wakiongozwa na Gavana
wa Lions Club katika nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini
bwana Hyderali Gangji wakiwa katika shule ya msingi Town...Madawati hayo
165 yametolewa na Lions Club ya mkoa wa Mwanza.Mwandishi mkuu wa
Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha 30 kilichojiri mwanzo
hadi mwisho.
Gavana wa Lions Club International katika
nchi ya Tanzania na Uganda na Sudani ya Kusini Hyderali Gangji alisema
wamekuwa wakitoa misaada mbalimbali mkoani Shinyanga ambapo mwaka jana
walitoa msaada wa chakula kwa wahanga wa mvua ya Mwakata wilayani
Kahama,pia chakula katika kituo cha walemavu wa ngozi cha
Buhangija,kutoa madawati katika shule ya msingi Town na Mwenge
Miongoni
mwa madawati ya chuma 165 yaliyotolewa na Lions Club International
katika shule ya msingi Town na Mwenge katika manispaa ya Shinyanga .
Mkurugenzi
wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akizungumza wakati wa hafla ya
kukabidhi madawati,ambapo mbali na kuipongeza Lions Club International kwa
kutoa msaada huo,aliwataka madiwani wa manispaa ya Shinyanga kufanya
kazi badala ya kukalia maneno maneno kwani kiongozi mzuri anapimwa kwa
maendeleo anayowaletea wananchi wake.
Miongoni
mwa madawati ya chuma 165 yaliyotolewa na Lions Club International
katika shule ya msingi Town na Mwenge katika manispaa ya Shinyanga .