Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu)
akizungumza na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji nchini (kushoto)
pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (kulia),
kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji wa kazi ndani ya Idara hiyo na
Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni Naibu Waziri wa
Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni. Wakwanza upande wa kulia ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya, na wakwanza upande wa
kushoto ni Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Victoria Lembeli.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya
akizungumza jambo katika kikao kazi alichokiitisha Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu) kuzungumza na
Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji nchini pamoja na Wakuu wa Idara wa
Wizara yake, kuhusu masuala mbalimbali ya utendaji kazi ndani ya Idara
hiyo na Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kulia meza kuu ni
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni. Wakwanza upande wa
kushoto ni Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Victoria Lembeli.
Kaimu
Kamishna wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli (wapili upande wa
kushoto) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles
Kitwanga (kushoto meza kuu) kuhusu masuala mbalimbali ya kikazi ndani ya
Idara yake katika Kikao kazi cha Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji
pamoja na Wakuu wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
kilichoitishwa na Waziri Kitwanga na kufanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kulia ni
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, balozi Simba Yahya.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto meza kuu), Naibu
Waziri wa Wizara hiyo, Injinia Hamad Masauni (kulia meza kuu) wakifurahi
jambo pamoja na Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji (kushoto) na Wakuu
wa Idara wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (kulia), wakati wa kikao
cha kujadili masuala mbalimbali ya utendaji kazi ndani ya Idara hiyo na
Wizara kiujumla. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Wakwanza upande wa kulia ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya, na wakwanza upande wa
kushoto ni Kaimu Kamishna wa Uhamiaji, Victoria Lembeli. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.