
Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji (katikati) akikata utepe
kuzindua rasmi Tawi jipya la Benki ya Amana, wakati alipokuwa
akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan kuzindua Tawi hilo lililofunguliwa leo Feb 25, 2016
Mbagala Zakiem jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Benki hiyo,
Dkt. Muhsin Salim Masoud (kushoto) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,
Abdallah Al- Nahdi. Picha na Sufianimafoto Blog


Naibu
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu Kijaji, akisoma hotuba yake ya
uzinduzi wa Tawi jipya la Benki ya Amana lililofunguliwa Mbagala Zakiem
jijini Dar es Salaam, ambapo Mhe. Kijaji alimwakilisha Mhe. Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwenye
uzinduzi huo.

Mkurugenzi
wa Benki Amana, Dkt. Muhsin Salim Masoud, akizungumza kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashantu
Kijaji, kuzindua Tawi hilo kwa niaba ya Makamu wa Rais Mhe. Samia
Suluhu Hassan.