
Baadhi ya watumishi wa TASAF
na Wadau wa Maendeleo wakiwa katika kikao kazi cha
tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya
Maskini ikiwa ni sehemu ya mapitio ya utekelezaji wa nusu mwaka .

Baadhi ya watumishi wa TASAF na Wadau wa Maendeleo wakiwa katika kikao kazi cha
tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa unusuru Kaya maskini

Mmoja wa wadau wa maendeleo
(aliyeshika kipaza sauti)
akichangia mjadala wa tathmini ya utekelezaji wa hughuli za Mpango wa kunusuru kaya
maskini unaotekelezwa na TASAF.

Baadhiyawatumishiwa
TASAF na wadau wa Maendeleo wakifuatilia maelezo ya tathmini ya
utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru
kaya maskini baada ya ziara ya maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni sehemu
ya tathmini ya Mpango huo inayofanyika makao makuu ya
TASAF.

MkurugenziMtendajiwa TASAF
,Bwana Ladislaus Mwamanga (kushoto) akijadiliana jambo na Kiongozi wa Benki ya Dunia nchini anayesimamia shughuliza TASAF,Bw.
Abdulah Mohamed Muderis (kulia) katika kikao cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za Mpango wa Kunusuru
Kaya Maskini kwenye ukumbi wa mikutano makao makuu ya TASAF-jijini Dar es salaam.
Mfuko
wa Maendeleo ya Jamii TASAF kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo
unaendelea na kikao cha kutathmini utekelezaji wa shughuli za Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini kinachofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Mfuko
huo jijini Dar es salaam.
Mkutano
huo unafuatia ziara zilizofanywa na wadau hao wa maendeleo na maafisa
wa TASAF katika mikoa ya DODOMA,MANYARA,SINGIDA,RUKWA na ZANZIBAR kuona
utekelezaji wa Mpango huo uliofanikiwa kuzifikia Zaidi ya kaya Milioni
Moja na Laki Moja nchini kote .
Kaya
hizo zimenufaika na ruzuku inayotolewa na TASAF kupitia Mpango wa
kunusuru kaya Maskini.Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho
Mkurugenzi Mtendaji Bwana Ladislaus Mwamanga amesema utaratibu wa
kufanya tathmini ya Mpango huo kwa kutembelea maeneo ya walengwa
husaidia kwa kiwango kikubwa kuona picha halisi ya mafanikio n ahata
changamoto zinazojitokeza ili kuboresha Zaidi huduma kwa walengwa.
Taarifa
kutoka maeneo yaliyotemebelewa na wadau wa maendeleo na watendaji wa
TASAF inayonyesha kuwa kumekuwa na mafanikio makubwa katika shughuli za
Mpango ambapo walengwa wameonyesha kuridhishwa na namna huduma za Mpango
huo zinavyowanufaisha hususani katika Nyanja za elimu, afya,lishe na
kuamsha ari ya kukuza shughuli za uzalishaji mali kwenye maeneo ya
walengwa.
Vikao
kazi hivyo vinatarajiwa kukamilika Ijumaa ya wiki hii kwa kufikia
makubaliano ya namna ya kuboresha Zaidi shughuli za Mpango wa kunusuru
kaya maskini.