
Mkuu wa wilaya ya Babati
Mkoani Manyara, Crispin Meela akiongea na vijana (pichani hawapo)
wakati wa uzinduzi wa semina ya mafunzo ya biashara kwa vijana
wajasiriamari
inayoendeshwa na Airtel chini ya mpango wake wa Airtel Fursa. Semina
hiyo ilifanyika Babati Mkoani Manyara. Pichani ni (kulia) Meneja huduma
kwa jamii , Hawa Bayumi, akifatiwa na Meneja Masoko Kanda ya Kaskazini
Brighton Majwala na Meneja mauzo wa Manyara,
Peter Kimaro

Mkuu wa wilaya ya Babati
Mkoani Manyara, Crispin Meela akimkabithi cheti mmoja ya washiriki wa
mafunzo ya biashara yaliyotolewa
na Airtel chini ya mpango wake wa Airtel Fursa wilaya ya Babati Mkoani
Manyara. Pichani ni (kulia) Meneja huduma kwa jamii , Hawa Bayumi,
akifatiwa na Meneja Masoko Kanda ya Kaskazini Brighton Majwala na Meneja
mauzo wa Manyara, Peter Kimaro.

Mkuu wa wilaya ya Babai
Mkoani Manyara, Crispin Meela akiwa katika picha ya pamoja na vijana
walioshiriki kwenye mafunzo ya biashara yaliyotolewa na Airtel chini
ya mpango wake wa Airtel Fursa wilaya ya Babati Mkoani Manyara.
Mkuu wa wilaya ya Babati
Mkoani Manyara, Crispin Meela amewataka vijana mkoani humo kuchangamkia
fursa ya mafunzo ya ujasiriamali
na msaada wa vifaa vya kuendeshea biashara vinavyotolewa na kampuni ya
simu za mkononi ya Airtel, kupitia mradi wake wa Airtel Fursa.
Meela ametoa wito huo mjini
Babati mkoani MANYARA, wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya Aritel Fursa ambapo zaidi ya vijana 200 wameshiriki mafunzo hayo.
Amewahimiza
vijana hao kubuni miradi inayohusiana na kilimo kwa kuwa sekta hiyo
ndio yenye uhakika wa kuajiri idadi kubwa ya watu hivyo kujikwamua
kiuchumi."Ni
lazima vijana muwe wabunifu na mjiunge kwenye vikundi vya wajasiriamali
ili muweze kutumia vizuri fursa zinazotolewa na Airtel pamoja na
serikali kufanyabiashara
kwa viwango vinavyokubalika" amesisitiza Meela.
Aidha
ameongeza kwa kusema mafunzo haya ambayo yanatolewa bure kwa vijana
yatachangia kiasi kikubwa katika kupata ujuzi na kuboresha uendeshaji wa
biashara zao na
kuongeza ufanisi. Na kuwapongeza sana Airtel kwa kuwekeza katika vijana
mbalimbali nchini.
Akizungumza
na vijana hao, Meneja huduma kwa jamii Bi Hawa Bayumi amesema kuwa
vijana wengi zaidi wanatarajiwa kufikiwa nchini kote katika awamu ya
pili ya mradi
huo.
Amesema
Airtel Fursa haitoi mikopo bali vijana watakaokidhi vigezo watapatiwa
ruzuku itakayotumika kununua zana zitakazotumika kuinua uzalishaji
katika miradi wanayoiendesha.
"Kuna
timu ya wataalamu watakaopitia miradi itakayowasilishwa ambao watapitia
vigezo vilivyoainishwa na washindi watasaidiwa vifaa ili ndoto zao za
kujikwamua kiuchumi
ziweze kutimia' Alisisitiiza Bayumi.
"Katika
awamu ya kwanza ya Airtel Fursa tuliweza kuwafikia vijana 2500 kupitia
mafunzo kama haya tunayoya fanya Leona vijana 13 walifanikiwa
wakawezeshwa kwa kupewa
vitendea kazi na hivi sasa wanafanya vizuri katika biashara zao"Amesema
AIRTEL imefanya utafiti nchi nzima na kubaini changamoto lukuki
zinazowakabili vijana ikiwemo ukosefu wa mitaji, ubunifu na elimu ya
Ujasiriamali ndio maana
ikaamua kuwekeza katika kundi hilo.
"Tunaamini
kuwa vijana watakao saidiwa watakuwa chachu ya kuwawezesha vijana
wengine kwa kuwaajiri na baada ya miaka michache vijana watakuwa
wamejikwamua kiuchumi
na kuondokana na umasikini" aliongeza Bayumi.
Amewashauri
vijana nchini kote kuchangamkia fursa hiyo kwa kujipatia elimu ya
ujasiriamali inayotolewa na kampuni yake ili waweze kufaidina mradi huu