Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani, Mhe. Balozi Simba Yahya
akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Magereza mara baada ya kuwasili
gerezani hapo kwa ziara ya kikazi Januari 29, 2016 kujionea ujenzi wa
mradi wa umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete lililopo Wilaya ya
Kilombero, Mkoani Morogoro(anayefuatia) ni Kamishna wa Sheria na
Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma Malewa.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya(wa
pili kulia) akiwa ameongozana na Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa
Magereza, Dkt. Juma Malewa(wa kwanza kushoto) kuelekea katika Ukumbi wa
Gereza hilo kwa ajili ya kupata taarifa kamili ya utekelezaji wa mradi
wa umwagiliaji Gereza la Kilimo Idete kutoka kwa Wakandarasi wa mradi na
Mshauri Mwelekezi mradi(kulia) ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilombero,
Bw. Yahya Sinaniya.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya
akiangalia sehemu ya banio la kutunzia maji ya mradi wa Gereza la Kilimo
Idete akiwa pamoja na msafara wa Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi(wa kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Kitengo cha
Manunuzi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Manyama Mapesi(wa pili
kushoto) ni Kamishna wa Sheria na Uendeshaji wa Magereza, Dkt. Juma
Malewa.
Muonekano
wa mfereji wa maji yatakayokuwa yakitumika katika mradi wa umwagiliaji
wa Gereza la Kilimo Idete, Mkoani Morogoro kama inavyoonekana katika
picha.
Mshauri
wa Mradi, Mhandisi Nzobonaliba Imani akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Balozi Simba Yahya(katikati)
alipotembelea mradi wa umwagiliaji wa Gereza la Kilimo Idete lililopo
Mkoani Morogoro(kulia) ni Mkuu wa Gereza hilo, Mrakibu Mwandamizi wa
Magereza, Nsajigwa Mwakenja wakiaangalia ujenzi wa mradi wa umwagiliaji
wa Gereza hilo.
Wakandarasi
wa Kampuni ya ujenzi wa mradi wa umwagiliaji wa Gereza Kilimo Idete,
lililopo Mkoani Morogoro wakiendelea na ujenzi wa mifereji ya maji kama
inavyoonekana katika picha.
Wajumbe
wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakipata maelezo
ya Kitaalam kutoka kwa Mshauri Mwelekezi walipotembelea mradi huo
kujionea hatua mbalimbali za ujenzi. Wengine ni Wajumbe wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Kilombero.
……………………………………………………………………….