Mwanzilishi
na Mkurugenzi wa Flaviana Matata Foundation (kushoto) na Meneja
Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi wakionekana
wenye nyuso za furaha baada ya kufunua kitambaa kwenye jiwe la msingi.
Meneja
Mwendeshaji wa Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi akikata utepe
kuzindua rasmi choo cha kisasa katika shule ya Msingi Msinune
kilichojengwa na Mo Dewji Foundation. Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule
ya Msingi Msinune iliyopo Bagamoyo, Msami Mgoto pamoja na wanafunzi wa
shule hiyo wakishuhudia tukio hilo.
Picha ya pamoja baada ya uzinduzi.
Taasisi
ya Flaviana Matata, imekabidhi choo katika Shule ya Msingi Msinune ya
Wilaya ya Bagamoyo, Mkoani Pwani kitakachosaidia wanafunzi wa shule
hiyo.
Tukio
la kukabidhi choo hicho limefanyika katika shule hiyo mapema leo na
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Flaviana Matata, Bi. Flaviana
Matata ambapo ameelezea kuwa, wamekua wakiwapatia wanafunzi wa Msinune
vifaa vya shuleni tangu mwaka 2014 na mwanzoni mwa mwaka jana aliombwa
kuwa mlezi wa Shule na kuweza kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili
shule hiyo ikiwemo suala hilo la vyoo vya waalimu na wanafunzi,
madarasa pamoja na nyumba za walimu.
Flaviana
amesema baada ya kuguswa aliweza kumshirikisha Mkurugenzi Mtendaji na
Rais wa Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji, alikubali
kutoa msaada huo kupitia taasisi yake hiyo ya Mo Dewji Foundation na
kuweza kujenga choo hicho chenye matundu nane.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Shule hiyo ya Msinune, Bw. Msami Mgoto ameshukuru
taasisi ya Mo Dewji kwa msaada wa kufadhili ujenzi wa choo hicho huku
akielezea kuwa itasaidia wanafunzi zaidi ya 300 wanaosoma hapo licha ya
kuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya majengo.
Naye
Mwenyekiti wa Kijiji cha Msinune, Ramadhani Mtokeni aliishukuru Taasisi
ya Mo Dewji kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Msinune huku akiomba
iendelea kuwasaidia pindi wanapokuwa na matatizo.
Kwa
upande wa mwakilishi kutoka Mo Dewji Foundation, Francesca Tettamanzi
amepongeza juhudi za Flaviana Matata za kusaidia jamii ikiwemo kukua
kwa elimu hapa nchini hivyo wataendelea kushirikiana naye bega kwa bega.
Francesca
ameongeza kuwa, Mo Dewji kupitia msaada huo, wanafunzi watakuwa katika
mazingira mazuri na safi kwa afya zao ikiwemo kusoma bila kuwa na tatizo
la awali la choo, kwa sasa na miaka ijayo choo hicho kitakuwa mkombozi
na msaada mkubw