Dkt.Magreth
William Magambo ambae ni Daktari Bingwa wa Mionzi katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure akitoa ufafanuzi juu ya Ushiriki wa
Watumishi wa Hospitali hiyo la kushiriki Usafi wa Mazingira la Kila
Jumamosi ya Kila Mwisho wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Amesisitiza
wananchi kuwa na desturi ya kufanya Usafi wa mara kwa mara (Kila Siku)
katika mazingira yao ili kuepukana na hatari ya kupata magonjwa ya
kuambukiza ikiwemo kipindupi huku akikumbusha zaidi pia wanajamii
kuzingatia kanuni za usafi katika maeneo muhimu kama vile vyooni. Kunawa
mikono kwa maji safi na sabuni baada ya kutoka chooni.
Dkt.Peter
Maziku ambae ni Daktari katika kitengo cha CTC katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure akizungumza wakati wa zoezi la
usafi la kila mwisho wa mwezi lililofanyika hii leo Jijini Mwanza.
Anasema watoa huduma mbalimbali (Madaktari, Waalimu, Wafanyabiashara nk)
katika jamii lazima wawe mfano wa kuigwa katika kuwajibika kuweka
mazingira katika hali ya usafi ili kuwezesha wananchi wengine kuiga
mfano huo.
Baadhi
ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure
wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho
wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Baadhi
ya Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure
wakishiriki zoezi la Usafi wa Mazingira la Kila Jumamosi ya Kila Mwisho
wa Mwezi lililofanyika hii leo January 30,2016.
Kulia
ni Dkt.Peter Maziku ambae ni Daktari katika kitengo cha CTC katika
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure akiwa pamoja na
Dkt.Charles Ludibuka ambae ni Mfamasia katika Hospitali hiyo Sekour
Toure walishiriki zoezi la usafi katika Mazingira ya Hospitali hiyo.
Katika picha wakichoma uchafu baada ya usafi.
chanzo:Na:George Binagi