Wiki iliyopita mmoja wa waanzilishi wa kundi la Mtu Chee, Country Boy alisema kuwa Young Dee amejiengua kwenye kundi hilo na nafasi yake imechukuliwa na Young Killer. Wiki hii kuna cover imeanza kusambazwa ya ngoma mpya ya Mtu Chee ambayo kweli wanaonekana Country Boy, Stamina na Young Killer.
Bongo5 imemtafuta Young Killer kutaka kufahamu kuhusu kuhusika kwake na kundi hilo kama amejiunga rasmi na kuziba nafasi ya Young Dee ama laa.
“Mimi sio kwamba nimejiunga na mtu Chee, yaani mimi sio msanii rasmi wa Mtu Chee” alisema Young Killer.
Msodoki aliendelea kuelezea uhusika wake katika wimbo mpya wa Mtu Chee;
“Mtu Chee tunafanya nao kazi lakini mimi sio mtu ambaye nimeingia kabisa kuziba labda nafasi ya Young Dee au nini, Mtu Chee wenyewe kuhusiana na sekta hiyo wanajua wenyewe, lakini mimi niliitwa kufanya kazi na ndo nafanya nao kazi lakini mimi kundi langu ni Matunzo Zero Unit ndio kundi langu. Mtu Chee nitaendelea kufanya nao kazi endapo watakuwa wanaaniita na kujumuika katika ngoma zao na ninawaheshimu kwasababu n
i ndugu zangu kwasababu wamenitangulia na ni watu ambao walinipokea vizuri katika muziki.”
Muda mfupi baada ya Young Dee kuhojiwa na 255 ya Clouds Fm ambapo alithibitisha kuachana na Mtu Chee, rapper huyo alipost screenshot ya kuonesha kuwa Young Killer amemu unfollow Instagram kitu kinachoashiria kuwepo kwa tatizo kati yao.
Haya ndio maelezo ya Young Killer kuhusu kum-unfollow Young Dee
“Kuhusiana na ‘Kum-mfollow mtu au kumfollow, sio sababu ya kuwa na tatizo kwasababu Instagam sisi tunafanya kazi au tunashauriana au studio au sehemu za show, Instagram ni sehemu tu ya kuangalia picha, kwahiyo mtu kumunfollow haimaanishi kunakuwa na tatizo ni maswala tu ya kawaida kwasababu hata yeye pia hajanifollow vilevile, kwahiyo haimaanishi kwamba tunakuwa tunabeef, Instagram haitufanyi sisi tukosane kwasababu tumeanza kufahamiana kabla ya Instagram.”
Kwa kumalizia young Killer amesema hana beef yoyote na Young Dee;
“Sina tofauti na Young Dee kwasbabau sijaingia kuziba nafasi yake au mbali na hapo sikuwa na tofauti yoyote kwasababu ni watu ambao tunafanya kazi tunawasaidiana kwa namna yoyote” alisema Young Killer.
“Ukaribu wetu bado upo kwasababau ni mtu ambaye tumeshirikiana kwenye kazi nyingi na tunakutana mara kwa mara, hata kwenye ngoma ya ‘Akili Za Usiku’ ni mtu ambaye tulishirikiana na kwenye video tulikuwa pamoja, hata ile ngoma ya Nyandu ‘Kwa Mafans’ na hata ngoma iliyotoka hapo nyuma ‘Tusamehe Mola’ ni ngoma ambayo tulishirikiana na tukaandaa show kwa pamoja.” Alimaliza