Oct 14, 2015

Nyota imenifundisha biashara ya muziki – Msechu


11313721_433097830210023_61469450_n
Peter Msechu amesema wimbo wake, Nyota umemfanya aelewe na kuamua kufanya muziki wa kibiashara tofauti na alivyokuwa akifanya huko nyuma.  Msechu ameiambia Bongo5 kuwa mwanzo alikuja hajaelewa siri ya mchezo.
“Nyota ndio imenifanya nielewe maana biashara ya muziki,” amesema. “Sasa hivi nitakuwa nazingatia kila kitu kwenye muziki wangu. Muziki ni biashara kama biashara nyingine, sio kutoa toa ngoma holela. Kwahiyo watu wasubirie mengi mazuri kutoka kwa Msechu.”

CREDIT: Bongo5