Vanessa Mdee amesema kuwa tuzo aliyoshinda AFRIMMA ya ‘Best Female East Africa’ huko Dallas, Marekeni weekend iliyopita ina maana kubwa sana kwake kwasababu imefungua ukurasa mpya katika muziki wake. Vee Money ambaye kwa mara ya kwanza tulimshuhudia akiibuka na tuzo ya AFRIMA mwaka jana huko Nigeria ikiwa ndio ya kwanza kimataifa, amesema tuzo aliyoshinda sasa ya AFRIMMA ni ujumbe tosha kwa wasanii wa kike wa Afrika.
“Ni tuzo ya pili kimataifa lakini ni ya kwanza ambayo inaashiria kwa wasanii wa nje ya Tanzania kwamba Vanessa Mdee sasa ni msanii ambaye tu natakiwa kumwangalia na kumheshimu, ni hatua nzuri na ukurasa mpya umefunguka kwenye career yangu ya muziki.”
Vanessa ameonekana kuwekeza zaidi kwenye muziki wake kwa kufanya video kali na collabo na wasanii wan je, kitu ambacho muda si mrefu kitamuongezea nafasi ya kuonekana zaidi katika soko la kimataifa.
credit: Bongo5