MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGWA MWILI WA MAREHEMU DKT. KIGODA KARIMJEE DAR.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania Abubakary Zubeiry, wakati
alipowasili kwenye Msikiti wa Maamur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam,
leo asubuhi kwa ajili ya kuswalia mwili wa marehemu Dkt. Abdallah
Kigoda, aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, aliyefariki dunia
majuzi Hospitali ya Apollo nchini India, alipokuwa amelazwa akitibiwa.
Marehemu Kigoda anatarajia kuzikwa leo Jimboni kwake Handeni, mkoani
Tanga.
Maafisa
wa Bunge wakibebea Jeneza lenye mwili wa marehemu Dkt. Abdallah Kigoda,
wakati ulipowasili kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam,
kwa ajili ya kuagwa.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akishiriki na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu, kumswalia Marehemu
Dkt. Abdallah Kigoda, aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, wakati
wa swala hiyo iliyoswaliwa kwenye Msikiti wa Maamur uliopo Upanga jijini
Dar es Salaam, leo asubuhi. Marehemu Kigoda anatarajia kuzikwa leo
Jimboni kwake Handeni, mkoani Tanga.