Oct 13, 2015

PINDI CHANA AMKABIDHI RAIS WA BARAZA KUU LA UN TAMKO LA KUTOKOMEZA NDOA ZA UTOTONI

 Mwenyekiti wa Mtandao wa Kimataifa wa Wabunge  (PGA) Mhe.  Pindi Chana ( MB) akimkabidhi Rais wa Baraza Kuu la 70 la Umoja wa Mataifa,  Bw.Mogens Lykketoft,Tamko la  wabunge lenye sahihi 607 za wabunge kutoka mataifa 70 la  kutokomeza ndo za utotoni na za kulazimisha katika hafla fupi iliyofanyika  Umoja wa Mataifa siku ya Jumatatu.
 Mwakilishi wa Kudumu wa Zambia katika  Umoja wa Mataifa, Balozi Dr. Mwaba Kasese-Bota akizungumza wakati wa hafla hiyo ambapo alianisha mipango mbalimbali inayofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwamo viongozi wa kimila katika kuzunguia ndoa za utotoni na za kulazimishwa.
  Mwakilishi wa Kudumu wa Ghana katika Umoja wa Mataifa, Balozi Martha Anna Akyaa Pobea naye akitoa mchango wa namna  gani serikali yake inavyolishughulikiwa   tatizo za ndoa za utotoni ambapo amesema katika nchi za Afrika Magharibi katika kila watoto watano wa kike, wawili  huolewa kabla  ya kutimiza miaka 18 na kwamba ndoa hizo za utotoni si tu kwamba zinadumaza  ukuaji wake lakini pia zinachaniga mimba za umri mdogo,  vifo vitokanavyo na uzazi,  maambukizi ya magonjwa mbalimbali na kuchangia  umaskini kwa watoto wengi wa kike.
 Sehemu ya  washiriki wa hafla hiyo  wakiwamo  watalamu kutoka Wizara ya  Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto wakiongozwa na  Kaimu Katibu Mkuu, Bi, Nuru Milao.

Na  Mwandishi Maalum, New  York
Mtandao wa Kimataifa  wa Wabunge kutoka  Mabunge mbalimbali  Duniani (PGA),  umemkabidhi Rais wa Baraza Kuu la  70 la Umoja wa Mataifa Bw. Mogens Lykketoft,  tamko   la kukomesha ndoa za utotoni  na za kulazimishwa kwa watoto wa kike.

Akikabidhi tamko hilo lenye sahini  Zaidi ya 607   kutoka nchi 70 Mwenyekiti  wa Mtandao huo wa wabunge,  Mhe. Pindi Chana na ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii,  Jinsia na  Watoto amesema, kukabidhiwa kwa tamko  hilo kwa  Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa  kunakwenda sambamba na  maadhimisho  ya siku ya mtoto wa kike ambayo   huadhamishwa  kila  Octoba ya mwaka.

Mwenyekiti wa  PGA, amesema wakati wa  hafla hiyo fupi iliyofanyika hapa  Umoja wa Mataifa, siku ya Jumatatu kwamba,  ushirikiano wa wadau mbalimbali hasa  wabunge , serikali na asasi za kiraia ni  muhimu sana ikiwa jumuiya ya kimataifa  inataka kuondokana na kumaliza tatizo la ndoa za utotoni na za kulazimishwa.