Rapper Daz Baba amesema anachojivunia katika muziki wake mpaka sasa ni kiwanja pamoja na muziki wake kuwa mfano kwa wengine.Daz ameuambia mtandao wetu kuwa haangalii anaingiza pesa kiasi gani ila anaangalia mchango wake kwenye muziki.
“Mafanikio yangu kwenye muziki ni kuwa na identity yangu. Muziki wangu umekuwa na mchango sana kwenye muziki huu. Kwenye masuala ya pesa nimenunua viwanja na mwaka huu nikipata pesa najenga. Unajua mafanikio sio pesa tu, ukiangalia ulipotoka na ulipo utajua mafanikio yako.”