Sio wasanii wa muziki pekee walioathirika kutokana na kampeni za siasa zinazosababisha wengi wao kushindwa kutoa kazi zao katika kipindi hiki cha uchaguzi, bali hata wasanii wa filamu.Muongozaji na muigizaji wa filamu za Bongo , Jacob ‘JB’ Stephen amewaomba mashabiki wake wavute subira kutokana na kushindwa kuiachia filamu yake mpya iitwayo ‘Chungu Cha Tatu’ licha ya kuwa tayari imekamilika.
Kupitia akaunti yake ya Instagram Jb aliandika;
“WADAU FILAM YENU UA CHUNGU CHA TATU IPO TAYARI…LAKINI KWA SABABU JOTO LA UCHAGUZI LIKO JUU NILIKUWA NAOMBA KWA RUKSA YENU NIITOE BAADA YA UCHAGUZI…AU MNASEMAJE…”
Hata hivyo baadhi ya wasanii hasa wa muziki wameendelea na ratiba zao za kuachia kazi mpya katika kipindi hiki, japokuwa kazi hizo zinakutana na changamoto ya joto la uchaguzi na kusababisha zisifanye vizuri sana.