Sep 27, 2015

Hussein Machozi adai kukosa management kumemrudisha nyuma


11887107_489827214528874_218821705_n
Hussein Machozi amewataka mashabiki wake kujua kuwa tatizo linalomkwamisha kupiga hatua zaidi katika muziki wake ni kukosa management. Akizungumza kwenye kipindi cha FNL cha EATV, Hussein alisema nguvu yake binafsi anayotumia ndio imeishia hapo alipo sasa.
“Watanzania wanataka ukitoa ngoma na ukiki jumla. Kumbuka kwamba nilipokuwa nikifanya vile nilikuwa kwenye management na sasa hivi nafanya mwenyewe kama mwenyewe. Kwahiyo mimi nguvu yangu mimi mwenyewe mtu mmoja kama mmoja ndio imesababisha kufika hapa nilipo. Labda wanishauri nitafute management au mtu anayejua kufuatilia muziki anisaidie lakini sio kublame na vitu kama hivyo.”