Linex Sunday Mjeda ameahirisha kuachia wimbo mpya ambao hapo awali alipanga utoke mwezi huu wa naneMuimbaji huyo wa ‘Salima’ ameitaja sababu ya kusogeza mbele tarehe ya kutoa ngoma mpya kuwa ni kutokana na producer anayehusika na utayarishaji wa wimbo huo ni Tudd Thomas, ambaye hivi karibuni alipata matatizo ya afya baada ya kuvamiwa na vibaka na kujeruhiwa.
Hii ni taarifa ya Linex kupitia ukurasa wake wa Instagram:
“Habari hii ni Kwa mashabiki na wapenzi Wa muziki wangu kutokana na producer wangu @tuddthomas kupata matatizo ya kuvamiwa na vibaka na kumjeruhi nimelazimika kupeleka mbele wimbo wangu mpya uliotakiwa kutoka mwezi huu tarehe za mwishoni na sitautoa tena mpaka hali yake itakapokua poa na atakapo rudi kazi kwa kudra za Mungu tayari nina wimbo mpya ambao natarajia kuutoa mwezi ujao Mungu akipenda kuhusu nimefanya na producer nani unaitwaje? Ntashoot na nani? na mengineyo tuombe uzima nitawajuza GET WEL SOON BRO”
na Bongo 5