Aug 19, 2015

Wanaoandaa mashindano ya kusaka vipaji waipe kipaumbele na Hip Hop – Asema Fid Q


Fidq
Fareed Kubanda a.k.a Fid Q amesema kuwa wasanii wengi wa Hip Hop huwa hawajitokezi katika mashindano ya kusaka vipaji kwa wingi kutokana na kuamini kuwa wanaopewa kipaumbele ni wasanii wa kuimba.“Wadau wanaofanya talent search waangalie namna gani wanaipa kipaumbele Hip Hop pia, haiwezekani wakawa wanashinda wa kuimba tu. Kwasababu hizo za msingi watu wengi wa Hip Hop watashiriki katika mambo haya.” Alisema Ngosha kupitia 255 ya XXL.
“Nimeangalia mashindano mengi nimeona kama watu wa Hip Hop wenyewe hawajitokezi, lakini ukitembelea vilinge vya Hip Hop kuna watu kibo wanachana bars za hatari mwanzo mwisho.” Aliongeza Fid.