WAKATI vyama vinavyounda Umoja
wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ukiwa bize kumtambulisha mgombea wake wa
urais, Edward Lowassa kwa mbwembwe mikoani, Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kinadaiwa kujipanga kimyakimya huku kikitekeleza mikakati yake
chinichini, Risasi Mchanganyiko limeambiwa.
Mmoja wa maofisa wa chama hicho kutoka
ofisi ndogo, Lumumba jijini Dar es Salaam, amesema hawatishiki na
‘amshaamsha’ inayoendelea mikoani katika kumnadi mgombea huyo wa Ukawa,
kwani wanajua kitu gani wanapaswa kufanya ili kujipatia ushindi kwenye
uchaguzi mkuu ujao
.
“Wala usiwe na hofu kaka, kama wao
wanajua hii, sisi tunajua huu, unafikiri wao wana akili kuliko sisi?
Usije ukadhani tumelala tunawashangaa, sisi tupo bize sana katika
mikakati yetu, ingawa tunafanya kimyakimya, waache wajisahau watashtukia
tunaibuka na ushindi wa kishindo kama kawaida,” alisema ofisa huyo,
aliyeomba hifadhi ya jina lake.
Alisema kinachofanywa na Ukawa hivi sasa
ni sawa na maigizo, kwani umati wa watu wanaojitokeza kwenye mikutano
yao, haimaanishi kuwa ni wapiga kura, kwani wengi wao ni mashabiki ambao
hata kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura,
hawajajiandikisha.
Mgombea urais wa Ukawa, Edward Lowassa
amekuwa akitambulishwa katika mikoa mbalimbali nchini na kujaza umati wa
watu wanaojitokeza kusikiliza hotuba zake, kitu ambacho awali,
kilidhaniwa kuwa kitu kinachowatisha CCM, ambao ndiyo chama dola kwa
sasa