
Mwenyekiti wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Dkt. John Pombe Magufuli kuwa ndie Mgombea Urais wa Tanzania.

Mwenyekiti
wa CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikumbatiana na Dkt. John
Pombe Magufuli, mara baada ya kutangazwa kuwa ndiye Mgombea Urais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi,
mchana huu hapa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Dodoma Convition Centre,
Mjini Dodoma. Viongozi wakuu wameenda kwenye kikao hivi sasa cha kujua
nani atakuwa Mgombea Mwenza wa Urais.
Ama
kwa hakika hayawi hayawi sasa yamekuwa,Mchakato wa kumpata mgombea
Urais ndani ya chama cha Mapinduzi (CCM) umefanyika hatua kwa hatua na
hatimaye kapatikana atakaipeperusha bendera ya CCM katika kiti cha Urais
kwenye uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika hapo baadae mwaka huu.
Ni
John Pombe Magufuli ambaye baada ya Wajumbe wa Mkutano mkuu wa chama
hicho kupiga kura kwa wagombea Urais Watatu ambao ni Dkt John Pombe
Magufuli ,Dkt Asha Rose Migiro na Balozi Amina Salum Ali.
Kura
zilipigwa jana katika Mkutano mkuu wa chama hicho ndani ya ukumbi wa
Convetion Center mjini Dodoma,na matokeo yake yametangazwa rasmi mapema
leo asubuhi kuwa jumla ya kura zilizokuwa zimepigwa zilikuwa 2422,kura
zilizoharibika zilikuwa 6 na kula halali zilipatikana 2416.
Katika
kinyang'anyiro hicho Dkt Asha Rose Migiro alipata kura 59 ambayo ni
2%,Dkt John Pombe Magufuli alipata kura 2104 ambayo ni 87.1 % na Balozi
Amina Salum Ali aliyepata kura 255 ambayo ni asilimia 10.5.
Kwa matokeo hayo,imetangazwa rasmi kuwa Dkt John Pombe Magufuli ndiye atakaibeba bendera ya CCM katika kuwania kiti cha Urais
Kwa matokeo hayo,imetangazwa rasmi kuwa Dkt John Pombe Magufuli ndiye atakaibeba bendera ya CCM katika kuwania kiti cha Urais