Mawaziri wa fedha kutoka nchi
zinazotumia sarafu ya euro wanarejelea mkutano wao pamoja na waziri wa
fedha wa ugiriki kuhusu makubaliano ya kutoa mkopo kwa nchi ya Ugiriki.
Wakati
wa saa tisa za mazungumzo mjini Brussels siku ya Jumamosi Euclid
Tsakalotos alishindwa kuzishawishi nchi zingine za ulaya kuwa Ugiriki
ina mipango mizuri ya kumaliza tatizo lake la deni.Serikali ya Ugiriki inaomba mkopo mpya wa karibu euro bilioni 70.
Ujerumani imekuwa ikidai kuwa Ugiriki itaondoka kwa muda kwenye nchi zinazotumia safaru ya euro hatua ambayo inapingwa na Ufaransa na baadhi ya nchi za ulaya zinazo ihurumia Ugiriki.
Mawaziri hao wanatarajia kuwa na mpango kabla ya mkutano wa viongozi wa nchi za ulaya ambao utafanyika baadye hii leo.
