yake imetoka), Remember Me pamoja na We Are On A Roll. Jambo jema zaidi ni kwamba nyimbo za Juliana Patrick ambae ni binti wa Kisukuma kutoka Isolo Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza ni kwamba zimepokelewa vizuri pia hapa nchini Tanzania. "Dear Diary is being played on Tanzanian radios!! Asanteni sana!! #DearDiary This is just the beginning". Juliana Patrick aliandika kupitia ukurasa wake wa Twitta akizishukuru radio za Tanzania kwa kuucheza Wimbo wake wa Diar Diary na kusema huo ni mwanzo tu. Kubwa zaidi Kibao cha Dear Diary kilipotoka tu mwishoni mwa mwaka jana kilipanda chati na kufikia Nambari mbili katika chati za muziki huko Texas nchini Marekani. Hakika ni wakati wako ewe Mtanzania kuungana na Juliana Patrick katika kuzidi kuufanya muziki wake usonge mbele zaidi ili nyota yake ya Muziki ipate kupamba moto na hatimae kuipeperusha Vyema Bendera ya Tanzania katika anga la muziki Kimataifa.
chanz: BINAGI MEDIA
