Jul 17, 2015

DKT MAGUFULI NA MH SULUHU WALIVYOPOKELEWA KWA SHANGWE ZANZIBAR JANA

Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwa kwenye gari la wazi pamoja na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan kwenye mitaa ya Michenzani Zanzibar.
Mhe. Magufuli aliwasili Zanzibar kwa lengo la kutambulishwa kwa wanachama wa CCM Zanzibar akiongozana na mgombea mwenza Mhe.Samia Suluhu Hassan ambapo wote kwa pamoja walipata kuwasalimia wananchi wa Zanzibar kwenye viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
 Maelfu ya watu wakiufuata msafara wa mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Mhe. John Pombe Magufuli aliyeongozana na mgombea mwenza Mhe. Samia Suluhu Hassan


 Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM Dk.John Pombe Magufuli akivishwa skafu na chipukizi wa CCM Zanzibar mara baada ya kuwasili Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
 Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM Mhe. Samia Suluhu Hassan akivishwa skafu na chipukizi wa CCM nje ya jengo la Afisi Kuu ya CCM Zanzibar.
(PICHA: ADAM MZEE)