Alisema
kuna idadi kubwa ya vigogo kutoka vyama vingine ambao tayari wameomba
kujiunga na chama chao na taratibu zinafanywa kutambulishwa.
"...tendo hili la leo la kuwakaribisha vijana hawa ni mwanzo wa
kuwatambulisha wanachama mbalimbali wakiwemo wabunge na viongozi wa
vyama waliojiunga nasi baada ya kuvunjwa kwa Bunge. Tayari tunao baadhi
ya watu waliokuwa wabunge na wameshajiunga nasi na mchakato wa
kuwatambulisha unaendelea katika maeneo mbali mbali nchini," alisema
Mtemelwa.
Naibu Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Msafiri Mtemelwa (kushoto)
akimtambulisha aliyekuwa Mwenyekiti wa kitengo cha vijana Taifa wa NCCR
Mageuzi, Deo Meck alipotangazwa kujiunga na chama hicho rasmi leo jijini
Dar es Salaam.[/caption]
[caption id="attachment_59599" align="aligncenter" width="800"]
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari
wakiwa kwenye mkutano wa ACT Wazalendo.[/caption]
Akizungumzia mchakato wa uchukuaji fomu kwa ajili ya kugombea nafasi
mbalimbali ndani ya chama hicho, Mtemelwa alisema Julai mosi mwaka huu
Chama Cha ACT-Wazalendo kilifungua rasmi pazia la uchukuaji fomu za
kugombea nafasi mbalimbali zikiweno za Udiwani, Ubunge na Urais.
Alisema tangu kuanza kwa uchukuaji huo wa fomu kumekuwa na mwitikio
mkubwa wa wanachama kuchukua fomu na hadi sasa kuna baadhi ya majimbo na
kata zina watia azma kuanzia wanne mpaka tisa jambo ambalo alidai ni
faraja kwa ACT Wazalendo.
"Kati
ya majimbo 265 yakiwamo majimbo mapya 26 yaliyoongezwa hivi karibuni na
Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), ACT-Wazalendo tumeshakuwa na waweka
azma zaidi ya mmoja katika majimbo 226 kwa nchi nzima na tunaamini mpaka
kufikia mwisho wa uchukuaji fomu ndani ya Chama majimbo yote 265
yatakuwa yanawatia azma mbalimbali wanaosubiri kupitishwa na chama kwa
ajili ya uchaguzi mkuu," aliongeza Naibu Katibu Mkuu huyo wa ACT
Wazalendo.
Alibainisha
kuwa kichama mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu kwa nafasi ya udiwani
ni julai 24, kwa nafasi ya Ubunge mwisho ni Julai 31 na kwa nafasi ya
Urais mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Agosti Mosi, 2015. "Kwa
ngazi ya Taifa Halmashauri kuu itakutana Agosti 13 kwa ajili ya kuteua
jina la mgombea Urais wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, pamoja na
kupendekeza majina ya wagombea Urais kwenye mkutano mkuu. Agosti 13,
Mkutano mkuu utamchagua mtu atakayepeperusha bendera ya Chama cha ACT
Wazalendo katika mbio za urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."
"Hivi
karibuni tumepokea taarifa kutoka katika miji ya Tarime na Rorya Mkoani
Mara kuwa kuna watu wanapita na kutangaza kuwa Chama chetu kimezuiwa
kushiriki Uchaguzi kwa muda wa miezi sita.
Tumebaini lengo la upotoshaji huu ni kuwakatisha watanzania tamaa juu ya
ukuaji wa Chama Cha ACT-Wazalendo pamoja na dhamira yake nzuri ya
kuirudisha nchi katika misingi iliyoachwa na hayati Mwalimu Julius
Nyerere.
"Tunawataarifu
wananchi kuwa Chama chetu kitashiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka
huu kwa kuweka wagombea wa nafasi zote na Chama hakitakuwa tayari kuona
sehemu yoyote ya nchi mgombea wa CCM anapita bila kupingwa," alisisitiza
Naibu Katibu Mkuu huyo wa ACT Wazalendo.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
na JIACHIE