Naitwa Wastara Juma kama watanzania wenzengu mnavyonifahamu mimi ni
muigizaji wa filamu na kazi nyingine zinazohusiana na kiwanda cha
filamu. leo niongee kitu ili watanzania wenzangu muelewe kwanini
nimeamua kujiingiza kwenye siasa, kikubwa kilichonisukuma kuingia kwenye
siasa ni jambo moja kubwa sana kwangu ambalo ni (WALEMAVU) .
Huwezi
kusimulia uchungu wa mwana wakati haujawahi kuzaa huwezi kumzunguzia au
kumtetea mlemavu hali ya kuwa hujui uchungu, matatizo na maumivu yake,,
Mpaka sasa nimeishi katika hali ya ulemavu kwa zaidi ya miaka 6 japo
kuna wengine wamezaliwa wakiwa walemavu lakini kwa mda mchache tu miaka 6
nimepata mateso makubwa sana kuanzia kimaisha, kisaikolojia na hata
kimiundombinu ya nchi yetu. Pamoja na umaarufu wangu wote lakini hakuna
shirika wala taasisi yoyote iliyowahi kunishika mkono japo jambo hili
halikuwa muhimu sana kwangu kwani naweza kujihudumia mimi na familia
yangu.
Jambo la muhimu kwa sasa na linaloniumiza sana ni kuona ndani ya nchi
yetu walemavu hawana thamani wala haki yoyote si Mahosptalini, Maofisi
ya Kiserikali, ndani ya vyombo vya Usafiri, makazini na hata majumbani.
Labda moja tu ndio nimeona walemavu wamepewa nafasi angalau ya kupita
kuelekea sehemu au kuingia na kukaa ni ndani ya jengo la Bunge tu hapo
Dodoma.
Ndani ya nchi
yangu walemavu wote tunachukuliwa kama ombaomba na hali hii imewakatisha
tamaa walio wengi mpaka kuamua kuingia mitaani na kuzunguka wakiomba
shilingi mia mia za kujikimu kimaisha.
Naumia sana
napojitizama mimi na kufikiria je leo hii nisingekuwa maarufu ningeishi
maisha gani? Napata jibu kuwa huenda na mimi ningetafuta kijana
akanikokota na baiskeli na kuanza kuzunguka mitaani kuomba omba.
Siamini kabisa
kama kweli ukiwa mlemavu na akili yako pia inalemaa la hasha bali
naamini kuwa serikali yetu haitutazami walemavu kama na sisi tuna haki
sawa na wengine na tunastahili kujumulishwa na kila kitu wanachipata
wasio na ulemavu. Kuanzia kielimu, kiafya, miundombinu na sehemu
nyinginezo.
Leo hii ni
aibu kubwa kuwa hata television ya taifa inayotoa taarifa ya habari kwa
nchi haina mtangazaji anae wahabarisha walemavu viziwi ambao nao
wanahaki ya kujua nchi yetu na yaliyojiri.
Leo hii ni aibu zinajengwa barabara lakini hazima sehemu ya kupita walemavu
Leo
hii ni aibu kuona shule nyingi za ulemavu kwanza ni za zamani halafu
hakuna hata vifaa vinavyoendana na dunia ya kisasa ya sayansi na
teknolojia
Ni aibu kuona hatuna viwanja vya michezo kwa walemavu wakati na sisi tunahaki ya kushiriki hata mashindano ya Paralimpic.
Nimejaribu
kuonyesha na kuwapigania walemavu wenzangu kupitia sanaa lakini nimeona
sauti yangu ni ndogo na haisikiki kokote sasa nimeamua kuingia kwenye
siasa ili nisamame na kuwapigania Walemavu wenzangu wasio na sauti nao
sawa na kuona machozi, maumivu na mateso yao nayafuta vipi na pia ili
niweze kufuta kiapo nilichoweka kwenye nafsi yangu baada ya kuona
tunapokelewa vibaya ndani ya nchi yetu wenyewe kwamba lazima siku moja
nitawapa furaha walemavu wenzangu kabla sijafa nitapigania haki zao za
msingi ili nao au tujione tuna haki sawa na wengine nimekaa na dukuduku
hili ndani ya miaka 5 sasa huu ni wakati wa kulitoa na kujitoa kwa nguvu
zangu zote kuhakikisha walemavu wanawekwa katika mazingira mazuri kama
nchi za wenzetu waishi vizuri na kufikia hata nusu yake tu basi nitakuwa
nimefikia lengo la kutetea haki za msingi kwa walemavu wenzangu sababu
hata mim ni muhanga nimetumia lugha nyepesi ili nieleweke sina tamaa ya
chchote ila sitakuwa sawa kufa bila kuwaweka wenzangu kwenye maisha ya
haki na sehemu sahihi kwa sasa kuonyesha nilichohahidi moyo wangu ni
bungeni najua kma si wew uliyelamaa basi ndugu rafiki jirani yako lazima
atakuwa kwenye hali hii hivyo watanzania kutumia nguvu zetu kunisuport
amtapoteza kitu bali mtaongeza msaada kwa wale wasijioweza asante kwa
kusoma ujumbe huu
Wastara Juma on Instagram