Ishu ya Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu kutopata ujauzito
imeshazungumzwa mara kadhaa na hata yeye mwenyewe alishawahi kujitokeza
na kuizungumzia lakini safari hii amelizungumzia kwa njia tofauti.
Wema ambaye pia ni muigizaji wa filamu, awali alisema sababu kubwa ya
kutopata ujauzito ni masuala ya kiafya lakini safari hii ametoa kauli
tata ambayo inahusiana na imani za nguvu za giza.
Wema ambaye alifunguka hayo hivi karibuni, anadai kuwa yawezekana marehemu Steven Kanumba anahusika kwenye suala hilo.
“Unajua hili suala la mtoto linanisumbua sana yaani
na linaniuma kwa sababu napenda watoto sana na pia napenda kuitwa mama,
nimehangaika sana katika kuhakikisha nafanikiwa katika hili lakini ndiyo
hivyo imeshindikana.
“Serious! Ilifika kipindi yaani nilikuwa nachukia nilipokuwa
nikiziona siku zangu, nilikuwa sipendi kukutana na hiyo hali kwa sababu
naumia sana lakini ndiyo hivyo baada ya kuhangaika sana inabidi
nimwachie Mungu tu. Nahisi kukata tamaa lakini bado sijakata tamaa.
“Watu wananiambia mimi bado mdogo kwa hiyo sitakiwi kuwa na wasiwasi
sana ila muda unakwenda, sasa nina miaka 27. Niliwahi kupata mimba mwaka
2008, aliyenipa alikuwa marehemu Kanumba, lakini baadaye ilitoka na
aliposikia hivyo (Kanumba) alikasirika kwa kweli.
“Lakini baadaye ikawa kawaida, hata nilipokuja kuachana naye, bado
alikuwa rafiki yangu na tulikuwa tunaongea vizuri na kupigiana simu kama
kawaida ila alikuwa ananiambia ‘unajua una deni, nakudai watoto wangu
na nitafanya juu chini ili unilipe’.
“Basi ikawa kawaida yake kuniambia hivyo, wiki chache kabla ya kufariki
aliniomba tuonane lakini haikuwezekana kutokana na ratiba zetu
kutofautiana.
“Kuna muda huwa nafikiri au mizimu yake inahusika katika hii ishu! (anacheka sana).
“Unajua ile mimba ya Kanumba hata mimi sikuwa tayari kupata mtoto wakati
ule, niliona ndiyo kwanza naingia kwenye mapenzi halafu ndiyo nimetoka
kuwa miss tu, sasa itakuwaje, lakini huwezi jua labda pengine kwenye
‘abortion’ walivuruga baadhi ya vitu ndiyo maana mpaka leo imekuwa
hivi.”
Udaku Specially/bongo movies