Baada ya wezi kumfanyia kitu mbaya kwa kumuibia vifaa kibao kwenye gari lake na kuliacha kama gofu, staa wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ameamua kufunga siku saba kwa ajili ya kuwashtaki wezi hao kwa Mwenyezi Mungu.
“Niko kwenye mfungo wa siku saba kwa ajili ya kuwashtaki wale walioniibia maana najua Mungu ndiye aliyenipa na hao walioniibia atawalipa sawasawa na ubaya wao, sijafanikiwa kumjua hata mmoja lakini najua Mungu anawajua na atawalipa kwa wakati wake,” alisema Nisha.
chanzo GPL