Liverpool imekubali kumsajili kiungo
wa kati wa Uingereza James Milner kutoka kwa kilabu ya Manchester City
kwa uhamisho wa bure.
Liverpool tayari imekubali makubaliano ya
kibinafsi na mchezaji huyo wa miaka 29 ambaye atajiunga na kilabu hiyo
wakati kandarasi yake itakapokamilika katika uwanja wa Etihad tarehe
mosi July baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kimatibabu.Milner ameshinda mataji mawili ya ligi ya Uingereza ,kombe la FA pamoja na kombe la ligi wakati wa miaka mitano aliyohudumu katika klabu ya Machester ity
Ameichezea Uingereza mara 53 na kufunga mabao manane msimu uliopita.
Milner alijiunga na City kutoka Aston Villa mwaka 2010 baada ya kusajiliwa kwa kitita cha pauni milioni 26 na aliyekuwa meneja Roberto Manchini.
BBC

