Jun 6, 2015

CHADEMA YATIKISA ARUSHA

 Staa wa Hip Hop Bongo, Joseph Haule 'Prof. Jay' akihamasisha wananchi kujitokeza kwenda kujiandikisha "NDUGU ZANGU WANA WA ARUSHA NA TANZANIA KWA UJUMLA TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA ILI TUJIHAKIKISHIE UHURU WA KWELI NA SIYO MATUMAINI"
 Mbuge wa Arumeru Mashariki, Mh. Joshua Nassari amewataka Watanzania kutambua muda wa mateso waliyoyapata kwa miaka mingi sasa yamefikia ukomo,"Njia pekee iliyobaki ndugu zangu ni kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura."
Mbuge wa Arumeru Mashariki, Mh. Joshua Nassari akionyesha  magari mawili ya wagonjwa 'ambulance'  alizozitoa kwenye jimbo lake.
 Wananchi walioudhuria katika mkutano huo wa chadema jana jijini Arusha.
Mjumbe wa Kamati Kuu na Mbunge wa Viti Maalum Mh. Grace Kiwelu aliwataka wanawake kuwa chachu ya mabadiliko kwa Taifa."MUDA WA KUDANGANYWA KWA KANGA UMEPITA TUJITOKEZE KUJIANDIKISHA ILI OKTOBA TUPATE UHURU WA UHAKIKA,WANAWAKE TUKIAMUA TUNAWEZA"
Mbunge wa Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema ambaye pia ndiye aliyeteuliwa na chadema Kanda ya Kaskazini kuwa kiongozi wa kampeni za hamasa ya kujiandikisha aliwaambia wananchi wa Arusha kuwa safari ndiyo imeanza sasa kuelekea majimbo yote 33 ya kanda ya kaskazini kuhakikisha Watanzania wanajiandikisha kwa wingi ili Oktoba wafanye maamuzi sahihi.
Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini "WATANZANIA WENZANGU HUU NDIYO MUDA MUAFAKA WA KILA MMOJA WETU KUJIANDIKISHA ILI IKIFIKA OKTOBA TUWE TUNAFANYA MAAMUZI YA UHAKIKA NA SIYO SAFARI YA MATUMAINI"
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Manyara, Mh. Pauline Gekul aliwataka Watanzania kujiandikisha na kuhamasishana kwa wingi  kwa kutumia simu, mitandao ya kijamii na vikao vya kijamii ili ifikapo Oktoba waiondoe CCM madarakani.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Mh Cecilia Daniel Paresso amewataka Vijana na Akina Mama kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha ili ikifika October waweze kufanta maamuzi ya UHAKIKA na sio ya maamuzi ya MATUMAINI. 
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha Mh Rebecca Mgodo amewataka wananchi kusoma nyakati"NDUGU ZANGU MIAKA YA MATESO KWA WATANZANIA SASAS IMEFIKA MWISHO, TWENDENI KWA UMOJA WETU TUKAJIANDIKISHE KWENYE DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURATUITOE CCM MADARAKANI"-Mgodo
Mwenyekiti wa Chadema Kanda Ya Kaskazini Mh Israel Natse akiwaongoza viongozi na Wabunge wa Chadema Kanda ya Kaskazini kuingia uwanjani huku wakiwapungia wanachama na wapenzi wa Chadema waliofika uwanjani vya kilombero (PICHA NA WOINDE SHIZZA)