
Benki
ya Exim Tanzania imezindua kampeni maalum ya kuhamasisha wateja wake
kufungua akaunti ya amana ya malengo (Fixed Deposit Account) ikiwa
sehemu ya mpango wa benki hiyo kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba
miongoni mwa watanzania.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa juma lililopita, Meneja Bidhaa wa Benki hiyo, Bw Aloyse
Maro alisema lengo kuu la kampeni hiyo ni kukuza utamaduni wa kuweka
akiba hapa nchini ili kuongeza tija kwenye maendeleo ya taifa.
"Kampeni
hii ina lengo la kukuza utamaduni wa kuweka akiba hapa nchini.Viwango
vya ushindani vinavyotolewa na benki yetu ndio chachu ya mafanikio
kwenye kampeni yetu hii kwakuwa kupitia akaunti hii wateja wetu wataweza
kunufaika zaidi kwa kupata kiasi kikubwa cha faida mrejesho kutoka
kwenye akaunti zao,’’ alibainisha Bw. Maro.
Katika
jitihada za kuonyesha dhamira ya benki hiyo katika kuhamasisha zaidi
ufunguaji wa akaunti hiyo, Bw. Maro aliongeza kuwa kampeni hiyo
itaambatana na zawadi za kila mwezi kwa wateja watakaokuwa wanafungua
akaunti hiyo.
"Zawadi hizi za kila mwezi ni pamoja na simu aina ya iphone. Pia tunatarajia kutoa zawadi ya gari kama tuzo kuu '' alitangaza meneja huyo kwa majigambo.
Bw.
Maro alisisitiza zaidi kuwa Benki hiyo inadhamira ya dhati katika
kuhakikisha kwamba wateja wake wanapata huduma na bidhaa bora zaidi za
kibenki huku pia akitumia fursa hiyo kuwashawishi wateja wa benki hiyo
kufika au kuwasiliana na matawi ya benki hiyo ili kupata maelezo zaidi
kuhusu kampeni hiyo.